Jumanne. 16 Julai. 2024

Tafakari

Jumanne, Oktoba 24, 2023

Jumanne, Oktoba 24, 2023,
Juma la 29 la Mwaka

Rom 5: 12, 15, 17-21;
Zab 40: 6-9, 17 (K) 8,9;
Lk 12: 35-38.


KUWA MWEPESI KUMKARIBISHA YESU

Yesu anagonga ndani ya moyo wako. Anakuja mara nyingi anatamani kuingia ndani kukaa na wewe ili aweze kuongea na wewe, kukupatia nguvu na kukuponya na kukusaidia. Swali la kweli la kujiuliza je, ni kwa kiasi ghani upo tayari kumpokea mara moja? Mara nyingi tunaona shaka kumpokea Kristo. Mara nyingi tunataka kwanza tufahamu mpango wetu kwanza kabla hatuja jikabidhi kwa Yesu.

Tunachopaswa kufahamu ni kwamba Yesu ni mwaminifu kwa kila Nyanja. Ana jibu la kila swali ambalo tunaweza kuwa nalo katika maisha yetu. Je, unaamini hili? Je, unakubali ukweli huu? Kama tutakubaliana na hili tutakuwa tayari kufungua mioyo yetu na kumpokea bila kusitasita na kupokea neema yake. Tutakuwa makini kweli kweli kwa kile ambacho Yesu anataka kutuambia sisi na neema ambayo anataka kutupatia.

Tafakari leo, upo tayari kiasi ghani kufungua mara moja kila aina ya ufahamu wa maisha yako kwa ajili ya neema na mapenzi ya Mungu. Mkaribishe ndani kwa furaha na shauku kuu na ruhusu mpango wake uendelee kujifunua katika maisha yako.

Sala:
Bwana, ninatamani kukuweka wewe katika moyo wangu utembee katika maisha yangu uzame ndani kila siku. Ninatamani kusikia sauti yako na kujibu kwa moyo wote. Nipe neema niweze kuitika vyema kama inavyo stahili. Yesu, nakuamini wewe.
Amina..

Maoni


Ingia utoe maoni