Jumamosi. 18 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Oktoba 21, 2023

Jumamosi, Oktoba 21, 2023.
Juma la 28 la Mwaka

Jumamosi kumbukumbu ya Bikira Maria

Rom 4: 13, 16-18;
Zab 105: 6-9, 42-43 (K) 8;
Lk 12: 8-12.


IMANI YA JASIRI

Nguvu na uwezo unajaribiwa zaidi ya kuwa na vyeti. Hii ni kweli pia katika Imani yetu. Sio wengi watakao simama katika kujaribiwa huku kwa Imani. Yesu analifahamu hili na anataka kutoa somo kamili katika Injili. Masharti yake kama vile, ‘Kama” “Lakini” yanamuonesha wito wake kwetu wa kuwa makini. Haongei kwa mafumbo wala mfano. Anataka Imani kamili kwa Mungu isiotikiswa na iwe na msukumo kamili katika kumfuata Yeye katika hali zote.

Kukubali kwamba wewe ni Mkristo kwa baadhi ya nchi inamaana umejitangazia kifo. Na sehemu nyingine, ina maana umejitangazia, mateso, kukataliwa baadhi ya huduma au kuto kuchaguliwa kwa ajili ya jambo flani. Ni katika hali hiyo pia kumkubali Kristo inaweza kuhatarisha mambo binafsi, usalama wako wa kifedha na umuhimu wako pengine. Lakini Yesu anasisitisa kwamba kama tunataka kukubaliwa mbinguni mbele ya Malaika watakatifu kama watoto wa kweli wa Mungu, tunapaswa kukiri ukweli huo mbele ya ulimwengu, hata katika mateso na kutengwa.

Kanisa lina wakumbuka watakatifu kwasababu hii. Utukufu wao ni matokeo ya Imani yao na kujitoa kwao katika maisha yao ya Ukristo. Wafiadini mmoja baada ya mwingine katika historia walitoa maisha yao kwasababu ya upendo wao kwa Kristo. Mmoja wa wafiadini hao aliyetoa mfano wa upendo wake kwa Yesu ni Mt. Inyasi wa Antiokia ambaye tuliadhimisha sikuu yake tarere 17 Oktoba. Sehemu ifuatayo ni sehemu ambayo mtakatifu huyu aliandika kwa wafuasi wake wakati akisafirishwa kwenda Roma kurushwa katika matundu ya simba. “…niache mimi niwe chakula cha wanyama wakali, kwani ndio njia yangu kwenda kwa Mungu. Mimi ni ngano ya Mungu ambayo inapaswa kusagwa kwa meno ya wanyama ili niweze kuwa mkate safi wa Kristo. Niombeeni kwa Kristo ili wanyama hawa waweze kuwa chanzo cha kunifanya kuwa sadaka safi ya Mungu.”

Maneno hayo yana uvuvio na yanaonesha kuwa na nguvu sana. Ni rahisi sisi kuyasoma na kushangazwa na ujasiri wake, na kuongea haya kwa wengine, kwa kushangazwa na kuamini ushuhuda wake. Lakini ni vigumu sisi kuvaa viatu vyake na kuwa na ujasiri mkubwa kama wa kwake. Ni rahisi kuongelea watakatifu wakubwa na kuwaelezea kwa wengine lakini ni vigumu kuwaishi. “Ni rahisi kabisa kutoa mfano ila kuwa mfano wenyewe sio lele mama.” (Mt. Teresa wa Calcutta)

Tafakari juu ya maisha yako mwenyewe leo. Je, unatoa ushuhuda na kumsuhudia Yesu katika ukamilifu kwa wengine? Tafakari leo pia hivi wewe unafurahia kusoma tu maisha ya watakatifu au unajaribu kuishi walivyo ishi? Kama hukufanya hivyo, omba ili maisha yao yaweze kukusaidia kubadili maisha yako mwenyewe.

Sala.
Bwana, tunakushukuru kwa zawadi ya watakatifu wakubwa, hasa mashahidi. Ninakuomba maisha yao yanifundishe kuishi maisha ya utakatifu kama wao. Ninaomba unipe neema na ujasiri wakuishi hivyo. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni