Jumamosi. 18 Mei. 2024

Tafakari

Jumapili, Oktoba 22, 2023

Jumapili, Oktoba 22, 2023
Dominika ya 29 ya Mwaka

SIKU YA UMISIONARI ULIMWENGUNI

Isa 45:1, 4-6;
Zab 95: 1, 3-5, 7-10;
1 Thes 1:1-5;
Mt 22:15-21


UMISIONARI KATIKA MOYO WA IMANI YA KIKRISTO!


Muktasari wa masomo yetu

(Isaya 45:1.4-6) - Kurudi kwa wana Waisraeli kutoka utumwani chini ya mfalme Cyrus haionekani tu kama alama ya huruma ya Mungu kwa watu wake bali kama alama ya Mungu kuwa Bwana wa wote.
(1 Thessalonike 1:1-5) - Hapa linabeba taarifa za kwanza za Paulo kwa Wakristo wa Thesalonike. Nia yake inaonekana kila mahali.
(Mathayo 22:15-21) - Katika hali ya kutaka kumtega Yesu aseme kitu ambacho kinaleta utengano, maadui wake wanamuuliza kama ni halali kulipa kodi kwa Kaisari au la?

Ulishawahi kujiuliza mtu anavyokuwa Mkristo, “kwanini Mungu asimpeleka tu Mbinguni?” jibu, ni kwamba Mungu anampango na kila mmoja wetu, umeumbwa ili utimize sehemu ya umisionari wako. Na umisionari uanaanza na maneno ya Yesu, Mathayo 4:18 “njoo nifuate mimi nitakufanya kuwa mvuvi wa watu”. Ni ishara wazi kwamba Yesu alivyokuwa anamuita mtu alikuwa hamuiti kuja kuishi maisha naye bila kazi, bali kwa maisha yaliojikita katika umisionari. Hakuwaita kwenda hekaluni, au kwenye Tora, bali maisha ya ufuasi uliotukuka. Katika Matendo ya Mitume 1:8 tunaona kwamba kabla ya Yesu kupaa aliwaita mitume wake akawaambia kwamba wao watakuwa mashahidi wake kuanzia Yerusalemu, Yudea, Samaria na miisho ya ulimwengu. Na katika matendo ya Mitume 2, Roho Mtakatifu alitolewaa kama zawadi kwa watu ili waweze kutangaza neno la Mungu ulimweuni kote. Tangu Pentekoste utume wa Mungu umekuwa ukiendelea kokote ulimwenguni. Utume huu unaenda kila mahali ukiwa unamuweka Yesu katikati. Utume ni kitu ambacho tunaitwa kila mmoja tuweze kushiriki zaidi na zaidi. Utume ni kutoa ushuhuda kuhusu Yesu kwa kile tunacho kiamini hasa kumpenda Mungu na jirani.

Mungu wa Biblia sio Mungu wa utengano. Yeye anatusafisha sisi kwanza na baadae anatutumia sisi tuweze kuusafisha ulimwengu. Hii daima imekuwa ndio njia ya Mungu. Wakati Mungu anavyotaka kubadilisha ulimwengu alimchagua Noah afanye kitu ambacho hajawahi kufanya kabla(kutengeneza safina) ili afanya ambacho hajawahi kufanya kabla (mvua). Wakati Mungu alivyotaka kuleta mabadiliko alimuita Abrahamu aache nchi yake mwenyewe. Wakati Mungu alivyotaka kuwaokoa waisraeli Misri alimchagua mtu mmoja ambaye alikuwa sio muongeaji sana, Musa na kumtuma kwa Farao. Wakati Mungu alivyo hitaji mtu wakuficha wapelelezi wa Jeriko, alimchagua Rahabu (kahaba). Wakati Mungu alivyotaka kumuua Goliathi alimchagua kijana mmoja mchungaji tu naye ni Daudi. Wakati Mungu alivyotaka kuwakoa wana Waisraeli waliobaki utumwani Babuloni alimchagua mshichana mdogo tu Ester.

Wakati Yesu alivyotaka kuwachagua wafuasi wake aliwachagua watu wa chini wavuvi na watoza ushuru, tena muongeaji sana Petro na wana wawili wa ngurumo akawaambia waache neti zao wamfuate. Shuhuda ni mtu ambaye anasema tu kile alichoona na kukishuhudia. Ndio hivyo. Wewe ni mtaalamu wa maisha yako. Unacho takiwa ni kushirikisha kile ambacho Mungu amefanya katika maisha yako. Sisi wote tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Barua ya Mt.; Pailo kwa Wathesalonike inahitaji uangalifu mkubwa “Maneno yetu ya Injili sio maneno matupu bali ni Nguvu”. Habari njema kama alivyo ihubiri kwa hawa wa Giriki kabla hawajafanya ugumu wa mioyo yao, kwanza lilipo pokelewa na likazama katika udongo mzuri na kuleta matumaini makubwa. Kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani ya Paulo na wale wote waliompokea, injili ya Kristo ilipata umwilisho katika maisha yao. Je, hivi sivyo tunayo tamani hali iweze kuwa kila mahali?

Je, sisi ni wapi tunapaswa kushirikisha habari hii njema,? Je huu si utume usio wezekana? Ni utume usiokwepeka. Tunaanzia wapi? Pale pale tunapoishi. Katika Yerusalemu yetu, kwa marafiki zako, kwa wafanyakazi wenzako, jirani, na watu wote walio karibu yako. Na hii ndio sehemu ya pili ya kufanya hilo, sio tu kwa walio katika Yerusalemu yangu, kuwaambia kuhusu habari njeama ya Kristo, tuna sehemu tunapaswa kwenda mbali kabisa na mazingira yetu , watu tofauti na tamaduni zako mwenyewe, mazingara yako, watu walio karibu nasi lakini waliotoka mazingira tofauti na yetu. Paulo anasema “Nimekuwa yote kwa watu wote, ili kwa njia moja niwaokoe wengine” (1Kor 9:22)

Sala:
Bwana, nipo hapa nitume mimi. Nitume mimi niweze kuwa shuhuda wako.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni