Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Oktoba 14, 2023

Jumamosi, Oktoba 14 2023
Juma la 27 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mama Bikira Maria

Yoel 3: 12-21
Zab 97: 1-2, 5-6, 11-12 (K) 12;
Lk 11: 27-28.


ULIMWENGU UNAOISHI NDANI YA MAMA MARIA

Injili ya leo inauhusiano na Lk 8: 19-21, ambapo inaongelea kuhusu Mama na ndugu wa Yesu walitaka kumuona, inatoa somo lilelile kwamba mahusiano ya njee si zaidi ya kusikia neno la Mungu na kulitii. Kwa Injili ya Luka, Maria amebarikiwa kuliko wanawake wote. Lakini pia amebarikiwa kuliko wanawake wote si kwasababu ya kumzaa Mwana wa Mungu tu bali ni kwasababu aliliamini neno la Mungu na kulishika. Kwahiyo Yesu alivyosema wana heri zaidi wanao lishika neno la Mungu na kulitenda, Maria ni wakwanza kabisa tena kwa uaminifu mkubwa kulishika Neno la Mungu na kulitenda, hivyo Yesu haku maanisha kumtenga au kumkataa Mama yake. Wale wote wanaolisikia Neno la Mungu na kulitenda wanabarikiwa. Bikira Maria alivaa vazi la Imani isio yumba yumba na alijikabidhi kwa Mungu.

Kama isivyowezekana kulitenga Kanisa na Kristo, ndivyo isivyowezekana kumtenga Maria na Yesu. Yeye ni mfano unaongara katika kulishika Neno la Mungu. Maria anatufundisha jinsi ya kukubali na kulishika Neno la Mungu, jinsi ya kuliweka katika ubinadamu wetu, kuliishi, kuliweka ndani, nakulifanya lizae matunda mema. Kulifanya likue, na kuchukua sura mpya ndani mwetu, hata wakati tusipo lielewa au wakati linatufanya tuteseke. Wana heri wanaosikia Neno la Mungu na kulishika.

Sala:
Bwana, Ninaomba nikusikie wewe ukiongea na mimi. Ninaomba nikutane na wewe nipokee neno lako takatifu. Ninaomba pia niliweke neno lako katika matendo katika maisha yangu pia, ili niweze kupata neema ulizo niwekea juu yangu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni