Jumamosi, Oktoba 07, 2023
Jumamosi, Oktoba 7, 2023
Juma la 26 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Bikira Maria Mama wa Rozari
Bar 4: 5-12, 27-29;
Zab 69: 33-37 (R) 34;
Lk 10: 17-24.
FURAHA KAMILI
Nabii Baruku anawapa watu wa Mungu matumaini wale walio msahau Mungu wa kweli na kuchokoza hasira yake kwa kutolea sadaka miungu mingine na sio yeye. Baruku anawaalika sasa watubu sasa na kumrudia mara kumi zaidi. Na kama watafanya hivi watapokea furaha ya milele na ukombozi.
Furaha hii kamili inatoka katika Injili ambayo unaweza kuisoma katika hali tatu.
1) Furaha ya huduma: wale sabini wamerudi na kutoa taarifa ya ushindi kwa Yesu. Aliwapa mamlaka ana nguvu ya kuponya, kufukuza pepo na kuhubiri neno la Mungu, na walifanikiwa sana! Wakiwa katikati ya furaha yao kubwa, walikuwa makini kumpa Mungu utukufu. Ushindi wao ulikuwa wa kumuangamiza na kumshinda shetani. Tunaitwa kuendelea na utume huo huo.
2) Furaha ya ukombozi: Yesu anawaonya wasije wakaenda kwasababu ya ushindi wao bali wafurahi kwasababu majina yao yameandikwa mbinguni. Pamoja na muujiza wao kuwa mkubwa, bado muujiza mkubwa kuliko wote ni roho iliopotea kurudi kwa Mungu.
3) Furaha ya utawala: furaha yetu kubwa haipatikani katika huduma yetu au katika ukombozi wetu, bali kuhesabiwa katika mamlaka na utawala wa Baba yetu wa mbinguni, kwani huu ndio msingi wa huduma yetu na ukombozi. Hapa tunamuona Mungu Mwana akifurahi kwa njia ya Roho Mtakatifu kwasababu ya mapenzi ya Baba! “Baba ndivyo ilivyokupendeza kwani yalikuwa mapenzi yako”.
Sala:
Bwana ninakuomba nipate furaha hiyo kwa huduma yangu na zaidi sana katika ukombozi kwa kujikabidhi katika kuyafanya mapenzi yako.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni