Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Oktoba 06, 2023

Ijumaa, Oktoba 6, 2023
Juma la 26 la Mwaka

Bar 1: 15-22;
Ps 78: 1-5, 8-9;
Lk 10: 13-16


RUDI KWA MUNGU!


Tunasikia leo maneno mazito kutoka kwa Yesu leo juu ya miji ambayo amehubiri kwa nguvu-Korazini, Bethsaida na zaidi Kapernaumu. Kama Yesu akitembelea jumuiya yetu leo atasema nini? Je atatoa onyo kama alivyofanya kwa Korazini na Bethsaida? Na je tutajibuje?

Kila sehemu alipo enda Yesu alifanya makuu kuwaonesha ni kwa jinsi ghani Mungu anawapenda. Korazini na Bethsaida walibarikiwa kwa kutembelewa na Mungu. Walisikia neno la Mungu, habari njema na kuona miujiza mikuu aliyo tenda Yesu kwa ajili yao. Lakini hawa watu waliosikia Injili hapa waliitika kwa mwaliko mdogo kabisa. Yesu anawaonya kwa kutokufanya kitu. Toba ni wito wa daima kwetu kutoka kwa Yesu na tunapaswa kuusikiliza.

Kutatokea nini tusipo sikiliza?
Kutakuwa na adhabu na hiyo adhabu haitatoka kwa Mungu bali itakuwa ni matokeo ya dhambi zetu wenyewe. Kwa mfano mtu ambaye ameshauriwa asitumie pombe, badala ya kusikiliza akadharau. Na baadae akazidiwa na pombe na kufa. Kuna mifano mingi, ambayo watu hawabadilishi mienendo yao na kujikuta wakipokea adhabu ambayo inasababishwa na matokeo ya dhambi yao wenyewe. Inatoka katika matokeo ya matendo yao wenyewe.

Toba inahitaji kubadili moyo na mwenendo wa maisha. Neno la Mungu ni uzima na lina okoa maisha yetu ya mwili na roho. Hasira ya Yesu ameilekeza kwa dhambi na yale yote yanayo tusonga tushindwe kutimiza mapenzi ya Mungu. Kwahiyo kwa nini tusibadilike na kuanza maisha mapya ya ukweli na mazuri? Kwa mapendo anatuita sisi tutembee katika njia ya haki, ukweli na uhuru, neema na utakatifu. Je, unapokea neno lake kwa Imani na utii au kwa mashaka na shingo upande?

Sala:
Mungu mkuu na mtukufu, angaza giza la moyo wangu, utupe sisi Imani ya kweli, matumaini na mapendo kamili. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni