Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Septemba 18, 2023

Jumatatu, Septemba 18, 2023
Juma la 24 la Mwaka

1 Tim 2:1-8
Zab 28: 2, 7-9
Lk 7: 1-10.


SISTAHILI!

Mtumishi wa Jemedari yupo karibu kufa. Anawatuma wazee wa Wayahudi wakatafute msaada kutoka kwa Yesu. Wazee hawa wanasema “anastahili kufanya haya kwaajili yako”. Yesu bila kusema kama huyu Jemedari anastahili au la, anaondoka nao na kufuatana nao. Wakati jemedari alivyotambua Yesu yupo njiani anakuja, anamtuma mtu mwingine, mmoja wa marafiki zake. Alitaka wamwambie Yesu “asijisumbue! Hastahili yeye angie chini ya dari lake”. Anakataa walichosema wazee! “Kwahiyo sikujiona nastahili kuja kwako” “hata sikujichukulia mimi nastahili kuja kwako” “sistahili”.

Sisi je? Ni mara ngapi umepokea msamaha? Je, umetambua kiini cha dhambi yako? Imani inaona kutokustahili kwa nafsi binafsi. Usidanganywe na wale wanaokuambia “wewe ni mtu mzuri unastahili sana”. Kama tungepata tunachostahili (kwa ajili ya dhambi zetu) ni hakika, tutaishia motoni.

Kwakujibu swali “Hujambo?” C.J. Mahaney anajibu kwamba “ni nzuri kama nastahili”. Sisi wote hatumstahili Yesu. Imani ya kweli inaona kutokustahili kwa mtu mwenyewe. Lakini licha ya yote, Yesu anaingia nyumbani kwetu, anagonga ndani ya mioyo yetu. Si kwasababu tunastahili, ila ni kwasababu anatupenda sisi… anatupa zaidi ya kile tunachostahili.

Sala:
Njoo moyoni mwangu, Ee Bwana na nakuomba upafanye sehemu yako yakuishi.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni