Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Septemba 11, 2023

Jumatatu, Septemba 11, 2023

Juma la 23 la Mwaka

MASOMO YA MISA
Kol 1:24-2:3;
Zab 61:6-7, 9;
Lk 6: 6-11


WIVU UNATUFANYA TUSIFIKIRI

Katika Injili ya leo tunasikia Yesu akimponya mtu aliyepooza mkono wakiwa katika Sinagogi siku ya Sabato. Tabia ya ubinafsi ya mamlaka ya Wayahudi, Waandishi na Mafarisayo hawakutaka waelewe mafundisho ya Yesu. Wakaanza kumshutumu. Walikuwa wakiji shughulisha zaidi na kushika Sabato, bila ya kutoa msaada kwa huyu mtu anaye teseka.

Walikuwa na uwezo wakuokoa mnyama aliye anguka kwenye kisima siku ya sabato kuliko kumuokoa mwanadamu mwenzao. Yesu alikuwa na hali ya kumponya mtu sio tu kimwili bali pia kumsamehe dhambi na kumpa neema, Amani na furaha.

Hawa watu wa dini wa kipindi hicho walikuwa wamejikita kwa ajli yao wenyewe tu, Yesu alikuwa akisifiwa zaidi ya wao wenyewe. Alikuwa akisifiwa zaidi na kuheshimiwa zaidi ya Mafarisayo na Waandishi hivyo wakapatwa na wivu. Dhambi ya wivu inatuongoza kwenye kutokufikiri vizuri na ujinga. Dhambi hii inatufunga macho na kujikuta tukisema mambo ya uongo. Na hili ndilo lililo wapata Mafarisayo.

Tafakari leo juu ya hali ambayo unaweza kuwa nayo kama hiyo ya Mafarisayo na waandishi. Tambua matendo yao yamewekwa kwenye maandiko ili tuweze kujifunza. Jitahidi kuondoa hali kama hii, kama unaona huna furaha ndugu yako anapo fanikiwa, na badala yake kumtengenezea vitu vya uongo ili kuchafua sifa yake, jitahidi kuacha kabisa. Furahia mafanikio ya wenzako ili Mungu akupe Baraka zaidi.

Sala:
Bwana, ninataka kuwa huru kutoka katika dhambi hii ya majivuno, wivu na uongo. Ninaomba unisaidie kuona hili katika maisha yangu, niziungame na badala yake niwe na huruma na mapendo.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni