Ijumaa, Agosti 25, 2023
Ijumaa, Agosti 25, 2023
Juma la 20 la Mwaka
___________________
Rut 1: 1, 3-6, 14-16, 22;
Zab 146: 5-10 (K) 1;
Mt 22: 34-40
___________________
KUMPENDA MUNGU KWA UFAHAMU WETU WOTE
Injili ya leo inatualika tutafakari njia iliyo kuu ambayo kila mfuasi wa Kristo inapaswa kuwa msingi wake. Upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani. Kwanza kabisa upendo kwa Mungu ni kushuhudia na kukiri upendo wa Mungu kwetu sisi. Sisi ni dhaifu sana na tunashindwa kumpenda Mungu kama inavyotupasa. Lakini ndani ya Yesu tunahisi upendo wa Mungu kwetu. Kwahiyo, kuhisi upendo wa Mungu, licha ya upweke wa mtu mwenyewe inamfanya mtu ampende Mungu kama matokeo ya kuhisi upendo huo. Huu ndio mwanzo wa kumpenda Mungu. Wakati mtoto anavyohisi upendo wa Mama, hafanyi kitu kinyume na Mama. Hii ndio maana ya kumpenda Mungu. Tukihisi upendo wa Mungu hatutafanya mambo kinyume na Mungu, hatujiingiza kwenye dhambi, bali tutafanya yote yenye kumpendeza.
Inamfurahisha Mungu tukiwapenda wengine. Kwahiyo, wakati mtu anampenda Mungu, anaanza kumpenda jirani pia. Je, ni muda ghani upendo wangu juu ya jirani unapokuwa kamilifu? Tunapowapenda ndugu zetu tunakuwa tunatamani na wao kila wakati wawe washiriki kwenye uzima wa milele. Tunakuwa tunatamani na kuomba kwamba waishi maisha yao yote katika neema. Kwahiyo wanakuwa washiriki wa uzima wa milele zawadi tuliopewa na Yesu. Tunakumbuka alichosema Yesu ‘mlicho watendea wadogo hawa mme mtendea yeye’. Tutoke njee ya nafsi zetu, tuweze kukutana na watu waliowahitaji, tuwasaidie kadiri ya uwezo wetu. Huu ndio upendo kwa jirani zetu.
Maandiko yanatuambia kwamba tunapaswa “kupenda kwa moyo wetu wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote” kwa njia nyingine kupenda kwa nafsi yetu yote. Je, unapampenda Mungu kwa nafsi yako yote? Unaweza kufanya hivyo tu kama tutakabidhi maisha yetu kwa Mungu. Kwa kila hali ulivyo? Mungu wetu mwenye uwezo wote na nguvu yote anapaswa kuwekwa katika hali ya juu ambayo haina mfanano na chochote. Kujikabidhi kwake itaweka mioyo yetu katika moto wake ! Hii inamaana kwamba tutamuona Roho Mtakatifu akifanya mambo ya ajabu katika mioyo yetu. Tutamuona Mungu akifanya kazi na kutubadilisha. Matokeo ya moto wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu, tutamuona Mungu akifanya mambo ya ajabu kwa wengine kupitia sisi. Tutamuona Mungu akiwa kazini na tutashangaa kwa anacho kifanya. Tutashangaa kwanza mkono wake wenye nguvu unaotenda kazi kupitia sisi. Je, unampenda Mungu kwa kila hali kwa jinsi ulivyo? Jikabidhi kabisa katika kumtumikia Mungu wetu na Bwana wetu na mapenzi yake matakatifu.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kukupenda wewe kwa moyo wote, akili zote na nguvu zote. Nisaidie mimi kukupenda wewe kwa hali yangu yote. Kwa upendo huo, ninaomba unibadili mimi niweze kuwa chombo chako cha neema. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni