Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Julai 04, 2023

Jumanne, Julai 4, 2023,
Juma la 13 la Mwaka

Mwa 19: 15-29;
Zab 26: 2-3, 9-12;
Mt 8: 23-27


KUTULIZA MAWIMBI NA YESU

Jaribu kufikiria ulikuwa katika mashua ndani ya bahari pamoja na Yesu na Mitume wake. Wewe ulikuwa mvuvi na ulikuwa ukitumia muda mwingi katika kuvua katika maisha yako. Siku nyingine mawimbi yametulia na siku nyingine mawimbi hayajatulia. Lakini siku hii ilikuwa ni ya pekee. Sasa siku hii mawimbi ni makali na unaogopa unaona kabisa huenda mambo yasiishie pazuri. Je, utamwamsha Yesu kutoka usingizini? Tutashindana na mawimbi bila kumwamsha yeye?

Yesu alikemea upepo wa bahari na hali ikawa shwari. Kama sentensi hii inamaanisha kutuliza bahari tuu, mmoja anaweza kujiuliza swali, kwanini Yesu hafanyi sasa? Kwanini anaruhusu wapendwa wake wakumbwe na mawimbi makubwa ya maisha? Je, hayupo tayari kutuokoa kama alivyo waokoa mitume? Kuna mambo makubwa zaidi kutoka sentensi hii, ni zaida yakutuliza tu bahari. Sehemu yeyote alipo Yesu pana utulivu, upole na Amani. Haijalishi ni kwa kiasi ghani maisha yanaweza kuwa mabaya na kukumbwa na mawimbi makubwa, uwepo wa Yesu tuu, unabadilisha hata kile tunachodhani hakiwezekana na hali ya utulivu hurudi tena. Tukiwa na Yesu katika boti yetu ya maisha hakuna mawimbi yatakayo tuangusha na kutupeleka mbali. Tatizo letu sisi tumekuwa watu wa Imani kidogo/hafifu. Imani yetu ni hafifu sana kiasi ambacho mambo yetu yasipoenda kama yalivyopangwa tunaanza kuwa na wasi wasi kuhusu uwepo wa Mungu ndani yetu. Ni kwa wale tuu waliojishika na Mungu na kuhisi uwepo wake ndani yao wanaosimama imara na kubaki vizuri bila kuyumbishwa. Watu hawa wanahisi Amani na utulivu katika hali zote, hata katika hali mbaya kabisa inayotisha katika maisha.

Yesu kwa huruma yake, anatusubiri sisi tumgeukie yeye katika hofu zetu na kutafuta msaada wake. Kama tutafanya hivyo atakuwa nasi na atakuwa kama mzazi kwa watoto wake wanao mwamsha wakati wa usiku kwasababu ya hofu. Na hakika na kwa upendo atakabili mawimbi hayo na hali itakuwa shwari na matumaini kuwepo tena. Tutatambua kuwa haya yatapita na kuwa imara tena. Hili ndilo somo kuu twaweza kujifunza kutoka katika habari hii.

Tafakari leo, ni kwa jinsi ghani tunakabiliana na magumu na shida katika maisha yetu. Yawe makubwa au madogo, je, unayakabili kwa ujasiri, utulivu na matumaini kwamba Yesu atakabili yote? Maisha ni mafupi sana hatupaswi kuishi katika hofu. Kuwa na ujasiri katika Bwana bila kujali nini ninacho kumbana nacho katika maisha yangu kila siku. Kama Yesu anaonekana amelala kwako, mwamshe tena kwa kutengeneza mienendo mizuri ya masisha ndani yake. Anatambua kuwa atafanya nini na utakuwa na hakika kwamba hataruhusu wewe uteseke kiasi ambacho hutaweza kuyakabili.

Sala:
Bwana, kwa kila njia unayoweza kupitia katika maisha yangu ninakuamini. Ninatambua upo daima na mimi na ninatambua kuwa huwezi kunipa matatizo makubwa kuliko yale ambayo naweza kuyakabili. Ninaomba uongeze Imani yangu ndani yako wewe, ili niweze kuhisi Amani na kusikia hali ya utulivu daima. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni