Jumamosi. 20 Aprili. 2024

Tafakari

Jumatano, Aprili 19, 2023

Jumatano, Aprili 19, 2023
Juma la 2 la Pasaka

Mdo 5:17-26
Zab 34:2-9
Yn 3:16-21


KUVUTWA KWENYE MWANGA!


Mungu Baba amemtuma Mwanae aje ulimwenguni kuwa mwanga wetu wote. Yeye ni Mwanga ambao unaondoa giza lote. Lakini Injili inasema kwamba “watu wamependa giza zaidi ya mwanga”. Wamechagua dhambi zao zaidi kuliko uhuru wa kutoka kwenye dhambi. Tv au magazeti huvutia watu zaidi wanapotoa habari za udhaifu wa watu, na watu hukimbilia hizi kwasababu ndicho chenye maana kwao. Kwasababu tunavutwa zaidi kupenda kusikia mambo ya giza kuliko ya mwanga.

Ni wazi kwamba sio kwa kila mtu. Walio wengi hawapendezwi na giza la ulimwengu pia na mambo ya kudhalilisha wengine. Lakini ukweli ni kwamba giza lipo mbele na tunapaswa kuwa makini kwasababu ya hali yetu yakuweza kuanguka. Tunapenda kwenda kwenye matope na kudhani tuna furaha.

Pasaka ni kipindi cha kuchunguza tunavutwa na nini zaidi. Je, tunajiruhusu sisi wenyewe kuvutwa kwenye mwanga? Je, tunavutwa na hali mbali mbali ambazo Mungu yupo karibu yetu hapa duniani? Lakini upo mvuto wa kutopenda mpangilio, nakuvutwa kwenye dhambi, mapambano ya ndani ambayo kila mtu yanamkuta. Pasaka ni kipindi cha kuwa makini na haya, kuya chunguza na kuyaona na kuamua kumchagua Yesu, kuanza kujenga maisha yetu ya fadhila kwa kuiga fadhila za maisha ya Yesu.

Kama wafuasi wa Yesu tunaitwa kuelekeza macho yetu kwake pekee. Tunapaswa kupenya giza kwa Imani na kuacha mambo yetu yavutwe kwa Yesu Kristo. Tujikite kwenye Mwanga katika kipindi hiki cha Pasaka. Tuache mwanga huu uongoze maisha yetu.

Sala:
Nisaidie mimi niweze kuishi kwenye mwanga. Nisaidie niweze kuelekeza macho yangu kuelekea kwenye utukufu wa ufufuko wako. Ninaomba furaha hiyo iweze kuondoa uharibifu wa mabaya ndani mwangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni