Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Aprili 15, 2023

Jumamosi, Aprili 15, 2023
Oktava ya Pasaka

Mdo 4:13-21
Zab 118:14-21
Mk 16:9-15


IMANI INATUONGOZA KWENYE UKWELI WA UFUFUKO!

Kukosa Imani kunamfanya mtu akose ukweli mwingi katika maisha. Imani juu ya uzuri wa ndugu zetu inatufanya tujenge ulimwengu kuwa sehemu nzuri ya kuishi. Imani juu yetu wenyewe inatufanya kuachia mawimbi mbali mbali yanayokuja kwetu tusio yafahamu. Imani juu ya utume wetu inatufanya tuishi vizuri wito wetu. Imani katika mapendo kwa Mungu inatufanya sisi tusiwe watu wazama za dhambi na kuwa “washindi wa wakati huu”. Imani kwa Yesu mfufuka inatusaidia tuweze kutangaza habari za ufufuko. Zaidi ya nyakati zote, ulimwengu wa sasa unahitaji watu wenye Imani.

Kwanini mitume walishindwa kuamini kwamba Yesu amefufuka kutoka wafu? Walikuwa wameshaona miujiza mingi sana kwa Yesu kabla ya kufa. Walimsikia akifundisha kwa mamlaka makubwa na neema. Na sasa, baada ya kufufuka kutoka wafu mioyo yao imekuwa migumu na hawakuamini mara moja. Yesu alibidi kuwatokea mara nyingi na kuonesha ushuhuda huo mbele ya macho yao. Walitaka kuamini lakini hawakuweza kuruhusu wao wenyewe kuamini ufufuko kwa Imani ya kweli mpaka Yesu atoe ushuhuda. Baada ya muda walitambua hata ushuhuda waliohitaji ulikuwa ndani yao.

Mara nyingi tuna alikwa na Yesu kuwa na Imani na kumwamini yeye na kukubali mambo mengi kwa Imani. Zawadi ya Imani ni sawa na moto mdogo ndani mwetu ambao mara nyingi kwa kutojali tunaruhusu uzimwe na mambo mbali mbali bila kukuwa. Nia ya Ukristo wetu ni kuruhusu moto huo ukuwe na kufikia kilele ambacho Mungu anapenda. Inawezekana kuwasha moto huo na kuwa mkubwa na hatimaye kuchoma chochote kinacho taka kuingia ndani. Njia ya moto huu unajali sana namna tulivyoshikilia ule moto mdogo ambao tayari umeshaingia ndani mwetu. Tunapaswa kuukuza na kuulinda ili ukuwe. Hili linawezekana kwa kuacha ulegevu katika kusali.

Sala ni ufunguo wa kumruhusu Mungu akue ndani mwetu. Yupo ndani, akiongea nasi na kutuita tuamini. Kila mara tunapo kaza macho katika moto huo, tuna uwezesha ukuwe na kuchukua nafasi. Na kama Wafuasi wangeweza kuacha tu zawadi hiyo ya Imani ikuwe wangeweza mara moja kumtambua Yesu na kumwamini mara moja, bila hata yeye kujidhihirisha kwenye macho yao. Je, unafanya nini katika maisha yako ili kuruhusu moto mdogo wa Imani uliopo ndani mwako kukuwa? Jikite daima kwenye sala, na tazama Imani yako kwa Yesu itakuwa na kungara.

Sala:
Bwana nakupenda wewe na nakuamini wewe. Ninakuomba unisaidie kukuza moto wa imani uliopandwa ndani mwangu uweze kukuwa. Nitakase moyo wangu kwa moto huu na niweke huru kutoka katika moyo wangu mgumu. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni