Jumamosi. 20 Aprili. 2024

Tafakari

Alhamisi, Aprili 13, 2023

Alhamisi, Aprili 13, 2023
Oktava ya Pasaka

Mdo 3:11-26
Zab 8:2,5-9
Lk 24:35-48


UFUFUKO: KUONDOA HOFU NA KUKUMBATIA FURAHA!


Wakati Wanafunzi wawili wakiwa wanashirikisha habari juu ya tukio la Emaus, Yesu alitokea kati yao, walishtuka na kuogopa. Yesu katika hali yake ya Kibinadamu yakuonesha makovu ya madonda yake, kwa kula chakula pamoja nao, iliwafanya waondoe hofu na kuondoa baadhi ya maswali yaliokuwa yakiwasumbua. Walimuona Yesu, Bwana wao mpendwa, ambaye amejifunua mwenyewe, ambaye ni muelewa, ambaye anawasiliana nao, ambaye anasamehe na ambaye anawapa nguvu. Waliyapokea maneno yake katika hali ya juu sana, na wanafanywa kuelewa habari yote kuhusu maisha ya Yesu. Watu ambao walifikiri kwamba maisha yao yamefika mwisho na ulimwengu wao umekwisha, walianza kuona mwanzo wa Ulimwengu mpya.

Hali hii ya Wafuasi inafunua hali ambayo hata sisi tunakutana nayo wakati Mungu anatuita tuingie katika utukufu na neema yake. Mara nyingi wakati Mungu anavyotuita karibu naye, wakati anatuita tuweze kuona furaha ua ufufuko, tunapatwa na mashaka. Tunaweza tukaona ngumu kupokea ukweli wa ufufuko katika maisha yetu. Hii inaweza kutokea kwasababu mbali mbali. Kukata tamaa inaweza kuwa sababu yetu kushindwa kukumbatia maisha ya ufufuko. Wafuasi walikatishwa tamaa kabisa kwa kifo cha Kristo. Na sasa kwamba amefufuka, na alikuwa amesimama mbele yao, walikuwa na wasi wasi kuachia hali hiyo ya kukata tamaa iondoke.

Sisi pia, tunaweza tukaacha uzito wa ulimwengu, dhambi zetu au dhambi za wengine, zitukatishe tamaa. Tunaweza kusikia hasira na kuchukia na tukajikuta tunashindwa kutoka katika matatizo tunayo kutana nayo. Kuwa na furaha ya ufufuko maana yake tunarudisha macho yetu na kuangalia ule ukweli ambao Mungu anapenda sisi tuutazame. Haina maana ya kukatishwa tamaa kwa matatizo mbali mbali yanayo kuja katika njia zetu. Au kushindwa kumfuata Mungu kwasababu ya dhambi za wengine. Mungu wetu anatuita tutazame kitu kingine kikubwa zaidi kuliko matatizo yetu. Anatuita kwenye ushindi wake. Kutazama katika ushindi wake ni kuwa huru na kuwa na Imani ya hali ya juu katika maisha yetu. Na Imani hiyo kwa Bwana mfufuka itakuwa na furaha ya ajabu ambayo Mungu anataka tuwe nayo. Kwa macho yake yakiwa yame elekezwa kwake, yote yale yanayo kushawishi ukate tamaa yataondoka.

Sala:
Bwana, ninataka kukutazama wewe. Ninataka kukuona wewe ukiwa umefufuka katika wafu na nichukue furaha kubwa katika ukweli huu. Nisaidie, niweze kuhisi furaha kuu inayotoka kwa kukujua wewe, Bwana wetu mfufuka. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni