Jumatatu, Machi 27, 2023
Jumatatu, Machi 27, 2023.
Juma la 5 la Kwaresima
Dan 13:1-9,15-17,19-30,33-62;
Zab 23: 1-6;
Yn 8: 12-20.
KUTEMBEA NA MUNGU
Tunakaribia pasaka, kipindi cha ufufuko wa Bwana wetu. Maada inayotawala katika masomo yetu ya leo ni vita kati wema na ubaya, uongo na ukweli. Sisi pia tuna vita kati ya wema na ubaya mioyoni mwetu, lakini mara nyingi tunapoteza muda mwingi kuwahahukumu wengine kuliko sisi wenyewe. Yesu anatuambia leo kwamba yeye ni mwanga wa ulimwengu, na hatuwezi kuwa katika giza kama tutamfuata yeye.
Mwishoni mwa injili ya leo, Yesu anakutana tena na Mafarisayo. Anawapa changamoto kwa kuongea ukweli kuhusu muunganiko wake na Baba yake na kuhusu nguvu na mamlaka aliyo nayo na utume anao paswa kufanya kwa muunganiko huu. Mafarisayo wanajaribu kumpa changamoto lakini Yesu anaamua kuongea ukweli kabisa tena kwa lugha iliyo nyooka kabisa bila kutumia mafumbo. Hakuna nguvu ambayo ilioweza kumshambulia Yesu iwe ya mafarisayo au ya mtu yeyote kabla ya “saa yake takatifu haijaja”.
Katika Injili ya Yohane, saa hii takatifu sio saa ya aibu na kukosa neema kwa Yesu, bali ni saa ya ushindi wake wa kweli juu ya dhambi na mauti. Katika hali ya kiulimwengu tunajua kuwa siku yake ya kukamatwa, na kusulubiwa na kutundikwa msalabani ni muda wa woga na hofu. Inaonekana kana kwamba mafarisayo walishinda na Yesu kupoteza. Lakini katika mtazamo wa Kimungu, ambao ndio mtazamo wa kweli, Yesu alitukuka kwa utakatifu. Ni wazi, Kwamba Mungu aliruhusu hali hii ya Mafariso kuwa chombo cha Yesu kujipatia utukufu kwa njia ya mateso katika wasaa wa Yesu. Katika hali ya Kimungu, wasaa wake hauwi muda wa kushindwa, bali, unakuwa muda wa ushindi mkubwa.
Muda sio mrefu tutaingia katika utukufu wa juma kuu, na kuona tena kwamba Baba anaruhusu Yesu aingie katika mateso makali yasio elezeka. Tunaona changamoto, na tuhuma za kukamatatwa kwake na ushindi wa uongo wa kutokuelewa wa viongozi wa Wayahudi. Anza kujiandaa katika kuingia katika wasaa huu wa Yesu na kungara katika ujasiri wa Imani. Tuangalie zaidi juu ya mwanga ulio ndani mwetu. Tutazame zaidi mtazama wa umilele zaidi kuliko mtazamo wa nje. Tusitazame zaidi ni kwa jinsi ghani tunafanya njia za msalaba nyingi zaidi, bali tujiangalie ni namna ghani tunaweza kujisafisha na kukunguta uchafu ndani mwetu na kujazwa na Mungu zaidi.
Sala:
Bwana, Baba amekutuma wewe kwa utume wa kutukomboa sisi na kuruhusu wewe uteseke na kufa. Lakini kwa njia ya mateso alinunua ushindi wa mwisho juu ya kifo na mauti. Nipe Imani niweze kuelewa ukweli huu kwa moyo wote. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni