Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Aprili 08, 2023

Jumamosi, Aprili 8, 2023
JUMAMOSI KUU:

KUSUBIRI KATIKA UKIMYA!

Kwa kifo chake, viumbwe vyote vilivyoumbwa vimefanywa upya. Dunia ilitetemeka, giza likaijaza nchi yote, jua likafifia (Lk 23: 44-45) kila kitu kipo katika utulivu. Leo Kanisa linatualika tusubiri kwenye kaburi la Bwana, tukitafari mateso yake, kifo nakushuka kwake kuzimu, tukisubiri katika sala na kutarajia ufufuko wake. Mama Maria yupo nasi, yeye ambaye aliyaweka yote moyoni mwake (Lk 2:19).

Leo hii katika miji yetu, kuna kelele za kila aina. Angani kuna kelele, barabarani kuna kelele, kelele nyumbani na hata katika Makanisa. Na zaidi ya yote kuna kelele katika akili zetu na mioyo yetu. Tunapaswa kujenga ukimya, kwasababu neno la Mungu halisikiki katika kelele za siku hizi. Hakuwezi kuwa na uhusiano wa kweli na Mungu kama hamna ukimya. Hakuwezi kuwepo na kukutana na Mungu kama hamna ukimya. Ukimya unatuaanda kukutana na Mungu na kumfuata. Katika ukimya Bwana wetu huongea nasi. Siku hizi watu wanaogopa ukimya hata katika sala, kanisani pakitokea uwepo wa ukimya, watu wanatufuta hata mbinu za kuondoa ukimya, kwamfano mmoja akisalisha akionekana kusubiri kidogo, mwingine hukimbilia mara moja, au padre akikaa kimya kidogo, mpiga kinanda naye hupiga ala fulani, je? Tunaogopa ukimya? Hili ni changamoto kwetu. Katika ukimya tutagundua mengi sana kuhusu nafsi zetu, udhaifu wetu, na uzuri wetu.

Tusubiri na Maria katika kaburi la Yesu. Yesu anatuambia kitu cha pekee na muhimu kabisa. Pengine ni kitu ghani…..? Ngoja nimsikilize kwa makini kabisa. Pengine ananiambia mimi, mwanangu NAKUPENDA SANA

Maoni


Ingia utoe maoni