Jumamosi, Machi 18, 2023
Jumamosi, Machi 18, 2023
Juma la 3 la Kwaresima
Hos 14:2-10;
Zab 81:6-11,14,17;
Mk 12:28-34
SALA NI KUJIONA MWENYEWE KWA NJIA YA JICHO LA MUNGU
Mungu anaenda kwa watu aliowachangua, mpendwa Efraim na Yuda, ambao wapo mbali na Mungu, waliokamatwa katika matatizo yao. Mungu alitaka watambue kwamba ingawaje ndiye yeye aliyewapa adhabu lakini pia ni yeye atakaye ponya magonjwa yao. Kama tutajitahidi kwenda kwa Bwana atakuja kwetu upesi kama vile mvua inavyo inyeshea ardhi. Lakini Mungu anaifahamu Efraim na Yuda na sisi pia. Fadhila yetu ni kama tone la umande ambalo hupotea. Uaminifu wetu ni mdogo na hafifu.
Mfano wa Yesu wa Mafariyo na watoza ushuru unaelekezwa kwao wote ambao hujiamini wenyewe kama watakatifu na kuona wengine wadhambi. Watu wawili walioenda hekaluni kusali. Mmoja anasimama mbele ya Mungu bila kujinyenyekesha na kusali kwa nguvu, huku akiwalaumu mwengine na kujiinua na kujitakia haki. Mwingine ni Mtoza ushuru anaye kakaa nyuma na kujiona mdhambi na kumwambia Mungu “unihurumie mimi kwani ni mdhambi”.
Je, tunasalije? Huwa tunamwambia Mungu ni kwa jinsi ghani tulivyowazuri na kutaka Mungu atusifie? Au je huwa tunaona uhusiano wetu wa kweli na Mungu? Kama ukweli wa Mungu ukitujaza sisi lazima tutajazwa na ukweli kuhusu dhambi zetu na ukosefu wetu wa mapendo. Sisi ni wadhambi na tunahitaji huruma ya Yesu hata katika kusali tunahitaji Roho atuongoze ili tuweze kumwomba Mungu vizuri.
Leo hii tunakazana kwa akili zetu wenyewe. Na tunajiona wenyewe kwamba kitu fulani ni hakika. Mungu anatuaona sisi kama tulivyo. Anaona mambo yote mazuri na yale ambayo tunapaswa kukazana kuyapigania. Anaona yale mambo ambayo yapo ndani kabisa mwa mioyo yetu, ambayo ni upofu katika maisha yetu. Mungu anatupenda kama tulivyo. Hivyo tujiangalie sisi wenyewe kwa jicho la mkombozi wetu. Tukijiona wenyewe kama Mungu anavyofanya tutakuwa tayari kupokea huruma yake na neema.
Sala:
Bwana, upendo wako unaniambia kwamba niungame na kurudi kwako. Kujitakia kwangu haki kunanifunga mimi nishindwe kuona makosa yangu. Ninaomba neema yako inisaidie mimi niweze kuona neema yako kama wewe unavyo niona mimi.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni