Jumanne, Machi 07, 2023
Jumanne, Machi 07, 2023
Juma la 2 la Kwaresima
Isa 1:10, 16-20;
Zab 50:8-9,16-17,21,23;
Mt 23:1-12
UNYENYEKEVU MBEGU YA KIMUNGU!
Leo nabii Isaya anawaambia wana Waisraeli wafanye uchaguzi. Wajioneshe wenyewe na waache kutenda maovu. Kwaresima ni kipindi cha neema kubwa, ni muda ambao tunapaswa kutafakari ni wapi tulipo kosea na kujaribu kurekebisha. Kama nimechukua fedha isio halali niangalie jinsi ya kurudisha. Kama nilikuwa mtu wa kuapa, niache na kubadilika. Katika hali yeyote, napaswa kufanya kitu. Naweza kuhitaji sakramenti ya kitubio au kutafuta upatanisho na mtu ambaye nilimuumiza au aliyeniumiza.
Yesu anatupa somo zuri sana katika Injili. Anatutaka sisi tuweze kutukuka! Anatutaka sisi tujulikane na wengine. Anataka mwanga wetu mzuri uangaze watu waweze kuuona na kwa mwanga huo waweze kufanya mabadiliko. Lakini anapenda hili lifanyike katika kweli sio katika hali ya kudanganya. Anataka ukweli wa “mimi” uangaze. Nao ni unyenyekevu. Unyenyekevu ni kuwa mnyofu na mwaminifu. Na wakati watu watakapo ona hali hii ndani yetu, watavutwa. Sio sana katika hali ya kidunia bali katika hali ya kibinadamu. Hawata tuangalia na kuwa na wivu bali, watatuangalia na kuona ukweli wenyewe na kuufurahia, kuutamani na kutaka kuuishi. Unyenyekevu unakusaidia ukweli kamili kuhusu wewe uweze kungaa. Na wewe ukiwa katika kweli unakuwa ndiye mtu mwingine ambaye wengine wanataka kukutana naye.
Sala:
Bwana, naomba unifanye niwe mnyenyekevu. Nakuomba niweze kuwa mwaminifu na mkweli kwa jinsi nilivyo. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni