Jumatano. 27 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Februari 23, 2023

Alhamisi, Februari 23, 2023
Alhamisi baada ya Jumatano ya majivu

Kum 30: 15-20;
Za 1: 1-4, 6;
Lk 9: 22-25


KUIPATA ROHO KWA KUPOTEZA ULIMWENGU!


Somo la kwanza kutoka katika kumbukumbu la Torati linatufundisha kushika Amri za Mungu kwa kumpenda Mungu, kwa kumtii na kutembea katika njia zake. Kama tutafanya hivyo, tutapokea ahadi zake, ambazo ni uhai na mafanikio. Kwa upande mwingine yule ambaye hamtafuti Mungu anakuwa amechagua kifo na uovu.

Injili inaongelea kuhusu kuchukuwa misalaba yetu na kumfuata Yesu kila siku. Luka anasisitiza “KILA SIKU”, kuonesha umuhimu wakujikita kila siku na kukumbutia misalaba inayopitia katika njia zetu kwa uaminifu na mapendo. Kukumbatia kile ambacho kinaleta uchungu, kisicholipa, kilicho chukiwa na ulimwengu sio rahisi. Hili ndilo alilolifanya Yesu kwa njia ya mateso yake, na kifo juu ya msalaba kwa ajili yetu, akashinda kwa ajili ya wokovu wetu.

Kuchagua maisha ya Imani na ukombozi wa roho zetu inatupasa kuacha mengi ulimwenguni humu. Tunapaswa kuishi katika hali ambayo inatuweka tayari “kuachia yote” hata kama yalikuwa kwa ajili ya faida yetu au kwa ajili ya ukombozi wa wengine. Hili ni ngumu kulifanya na linahitaji mapendo makubwa kwa Mungu. Inatakiwa tuwe tumeridhia wenyewe kutoka ndani, kiasi kwamba kuona utakatifu ni zaidi ya kitu kingine chochote. Usisite kumfanya Mungu kuwa kiini na lengo la maisha yako. Kipindi cha kwaresima ni kipindi muhimu sana cha kuingia ndani na kutazama mitazamo yako na tamaa yako na lengo la maisha yako katika hali ya juu kabisa. Mchague Mungu awe zaidi ya yote na wala hutajutia kufanya kufanya hivyo.

Sala:
Bwana, tunapoingia katika kipindi hiki cha kwaresima, nipe neema niweze kutazama juu ya malengo yangu. Nisaidie niweze kuchagua kile kilicho cha muhimu kabisa na kiini cha maisha yangu. Nisaidie nikuchague wewe zaidi ya yote katika maisha yangu ili unisaidie kuendana na mapenzi yako matakatifu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni