Jumatatu, Februari 20, 2023
Jumatatu, Februari 20, 2023
Juma la 7 la mwaka wa Kanisa
YbS 1: 1-10;
Zab 93: 1-2, 5;
Mk 9: 14-29.
NGUVU YA AJABU YA IMANI!
Swala wa Kiafrika anauwezo wa kuruka juu uwezo wa 10ft, ingawaje anaonekana ni kiumbe mdogo, mwenye urefu wa 3-4ft, katika mbuga za wanyama au zuu, wanajenga ukuta wa urefu wa 4ft kwenda juu. Kwanini? Ni kwasababu swala hawezi kuruka kizingiti bila kufahamu na kuona miguu yake itatua wapi baada ya kuruka. Ni kweli pia ukilinganisha na imani yetu kwa Mungu. Tunakuwa na imani tu pale tunapo elewa kitu.
Kuna sentensi yenye kushangaza kutoka katika Injili ya leo anayo ongea mtu mmoja. Alimwambia Yesu “nina imani. Nisaidie kwa imani kidogo nilio nayo!”. Kwamba huyu mtu alimfahamu Yesu kabla au la ni vigumu kusema. Bali aliweza kutoa ufupisho wa kitu ambacho ni kipingamizi kikubwa kwetu Wakristo katika kukuwa katika maisha ya Kiroho, ambayo ni imani yenye mashaka, imani isio kamilika. Huyu mtu alisema ukweli na undani wake kwamba, ingawaje ana amini ambacho Yesu anaweza kusema na kufanya, lakini bado amejazwa na mashaka. Alikuwa akianguka kwenye imani yake yenye wasi wasi. Na kwasababu alikuwa akikabiliana na ukosefu wake wa imani, alipata baraka nyingi. Sentensi iliosemwa na mtu huyu ilikuwa sentensi ya uaminifu. Ilikuwa ni sentensi ya kujali na pia ukweli wa imani yake.
Kama tunataka kukuwa katika Kristo, ni vizuri kutambua na kukiri kwamba huenda hatumuamini Yesu vizuri kama inavyo paswa au kama tunavyopenda iwe. Kitu kizuri na cha kweli ni kusimama mbele ya Yesu na kukiri kutoka ndani kabisa mwa mioyo yetu kwamba “ninakuamini Bwana, ila nakuomba unisaidie na kutokuamini kwangu”.
Sala:
Bwana, ninaomba nije kwako katika hali zote. Ninaomba nikupende na kukutumikia wakati maisha yakiwa mazuri, wakati maisha yana mawimbi na misuko suko na changamoto. Niongezee imani na unisaidie niweze kuidhihirisha imani hiyo katika maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni