Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Februari 17, 2023

Ijumaa, Februari 17, 2023
Juma la 6 la Mwaka wa Kanisa

Mwa 11: 1-9;
Zab 33: 10-15;
Mk 8:34 – 9:1.


KUMFUATA YESU!


Katika Injili ya leo Yesu anatuambia sisi wafuasi wake tubebe misalaba yetu tumfuate. Kumwamini Yesu, si kukubali mafundisho yake tu kuwa ni ya kweli na ya kuaminika, bali kuyatenda. Katika hali ya kawaida, kila mtu aliyesoma Injili ya leo atakuwa amejibu swali hili katika hali tofauti ya maisha yake. Kila wakati uendapo kanisani, unapo tumia muda kusali, au kusoma Maandiko Matakatifu kwa njia moja au nyingine, hata mara nyingi tumesali sala mbali mbali tukiweka akili zetu kuamua kumchagua na kumfuata Kristo. Lakini tunapaswa kufanya zaidi ya kufanya uchaguzi wa kiakili tu katika ujumbe wa Injili hii.

Neno, “Kila apendaye” linaonekana kufunua zaidi ya kuamua tu, linaonesha pia kutamani. Linaonesha kuwa ile tamaa ya kumfuata Yesu sio kila wakati ni hatua ya kwanza katika kumwelekea, ni ya mwisho. Hatua ya kwanza inapaswa kuja katika hali ya kuelewa ukweli na kuukiri. Pili, tunapaswa kufanya kile tulicho chagua. Tatu, wakati neema imeanza kufanya kazi ndani yetu tunaanza “kutamani” yote anayotaka Yesu kwetu na yote aliotuitia tuyafanye. Kwa hiyo ni uamuzi ghani tunao jikuta sisi wenyewe tukifuata tunapo amua kumfuata Yesu kwa moyo wetu wote? Tutajikuta tukitamani kile alichofunua Yesu, kujikana wenyewe, kuchukua misalaba yetu na kufuata nyayo za Yesu. Je, unatamani hicho?

Ni rahisi kutamani kupenda na kupendwa, katika hali ya kawaida kabisa. Ni matumini kwamba, sisi wote tunapenda kufurahia maneno ya ukarimu na maneno ya kujali, tukiyatoa na kuyapokea. Lakini kwa upendo wa Yesu unahitaji kufuata mfano wake wa upendo, unapenda wewe upende zaidi kuliko hata kujipenda mwenyewe, upendo wa sadaka. Huu ndio ukamilifu wa upendo! Tunaitwa, kupenda bila kuangalia gharama, bila kujali malipo tunayopata. Au pia katika hali ya juu kabisa tunaitwa kupenda hata kile kinacho tusababishia maumivu na ugumu inapofika ni kutimiza mapenzi ya Mungu. Mapenzi yake yanahitaji matendo ya sadaka. Upendo wa kweli unafanya hata zaidi ya haya.

Je, unapenda kumfuata Yesu na upo tayari kukumbatia yote anayotaka tuyafanye. Sema “ndio” kwake na msalaba wake. Mwishoni utapata uzima na furaha ya milele.

Sala:
Bwana, ninatamani msalaba wako. Ninataka kufikia kiwango cha upendo ambao utanifanya nijikabidhi kwako kabisa, bila kuhesabu gharama, na kutamani matendo yanayo hitaji sadaka kubwa. Ulibeba msalaba wako bila kujibakiza kwasababu ya upendo wako kwetu. Nisadie niweze kuiga mfano wako kamili. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni