Jumapili. 28 Aprili. 2024

Tafakari

Jumatatu, Februari 06, 2017

Jumatatu, Februari 6, 2017.
Juma la 5 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt.Paulo Miki na Wenzake mashahidi

Mwanzo 1: 1-19;
Zab 104: 1-2, 5-6, 10, 12, 24, 35;
Mk 6: 53-56.


KUKIMBILIA KWA YESU

Katika Injili ya leo tunasikia kwamba, wakati Yesu alipopita katika nchi ya Genesareti, watu wengi walimwendea ili waweze kupokea baraka na uponyaji kutoka kwake. Watu wa Genesareti walikuwa ni watu waliojaa imani thabiti. Kabla ya hapo walisikia kuhusu Kristo na walimjua kabisa. Alipopita njiani katika kijiji chao, walimkaribisha kwa mioyo mikunjufu tofauti na Gerasene mji wa jirani, ambao walimwomba aondoke katika mji wao alipotoa pepo wachafu na kuwaamuru wawaingie nguruwe, ambao walitoweka majini. Walikuwa sio watu wakufikiri sana ambao walithamini zaidi kundi la nguruwe kuliko huyu Mwokozi wa ajabu. Je, vipi kuhusu mimi? Ni tunu gani Yesu anakushikia wewe?

Hali hii inapaswa kuwa aina yetu ya kumfuata Yesu katika maisha ya imani. Tunapaswa kumtambua yeye kama mwanzo wa uponyaji wetu, hasa wa Kiroho, na tunapaswa akili zetu kumwelekea yeye kama Daktari ya Kimungu. Hamu yetu ya kumtafuta na nguvu vinapaswa vizidi kila kitu.

Tujitahidi sisi wenyewe kujiweka katika hali hii ya Injili, tukiishi huku tukitaka kuwa na nguvu zaidi na mwelekeo mkubwa katika hamu yetu ya kuwa na Yesu. Yeye ni chanzo cha neema zote na msamaha, na yeye ni mganga wa Kimungu anaye kusubiri wewe na mimi kwenda kwake tukiwa na mahitaji yetu ya kila aina. Tufanye bidii ya kumwelekea yeye na tumruhusu atumiminie neema zake.

Sala: Bwana, ninaomba uongeze hamu ya kukutafuta na kuwa nawe. Nisaidie niweze kutambua kuwa wewe ni Mganga wa Kimungu amabaye roho yangu inamtamani. Nisaidie niweze kukusadiki daima, nikija kwako kutimiza mahitaji yangu yote na tamaa ya kuwa nawe. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni