Alhamisi, Februari 02, 2023
Alhamisi, Februari 2, 2023
Juma la 4 la Mwaka wa Kanisa
Sherehe ya Kutolewa Bwana hekaluni.
Mal 3: 1-4;
Zab 24: 7-10;
Ebr 2: 14-18
Lk 2: 22-40.
KUJIWEKA WAKFU KWA BWANA!
Katika somo la Injili, Luka anaeleza taratibu tatu za sheria ambazo Maria na Yesu walijiweka. Siku nane baada ya kuzaliwa kwake, Yesu alitahiriwa. Alafu siku 33 baadae, Mama yake alimchukua Yesu Hekaluni kwa kazi mbili. Kwanza, kumtolea mtoto Yesu kwa Mungu, na alimtolea tena kwa kutoa shekeli tano. Hii ni mila ambayo ilikumbusha yote kuhusu kutolea sadaka kwa ajili ya kuokoa watoto wa kwanza wa kiume wa Israeli kutoka katika yule malaika wa kifo katika usiku wa Pasaka ya kwanza huko Misri. Pili, Maria alitolea sadaka ya mila yao ya kumtakasa na damu ya mama wakati wa kuzaliwa kwa mtoto.
Mila hizi tatu-kutahiriwa, kutakaswa baada ya mtoto kuzaliwa na sadaka ya kumuokoa mtoto wa kwanza wa kiume-vinaelekeza jinsi Mwanadamu hali yake ilikuwa ya dhambi. Kwasababu ya dhambi, Mwanadamu aliye anguka alijitenga na Mungu na alistahili tu baada ya kuhukumiwa na Mungu. Mila hizi zilionesha ulazima wa kukombolewa na kutakaswa. Mkombozi wetu alipitishwa katika mila hizi ingawaje hakutenda dhambi wala hakuwa na dhambi. Aliingia katika mila hizi kama mtoto, kama alivyokuwa mtu mzima na akaruhusu kujikabidhi kwaYohane Mbatizaji abatizwe ingawaje hakuwa na dhambi. Alifanya haya si kwasababu alihitaji utakaso wake mwenyewe bali alionyesha mshikamano wake na wadhambi ambao amekuja kuwakomboa. Kwa kufanya haya, Yesu alichukua udhaifu wetu juu ya nafsi yake mwenyewe kwa ajili ya wale aliokuja kuwakomboa. “Kwasababu alimfanya Yeye ambaye hakujua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili tuweze kuwa watakatifu wa Mungu kwa njia yake” (2 Kor 5:21). Wakati Maria anatolea “sadaka ya dhambi” na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya utakaso, alileta sadaka ya mtu maskini njiwa wawili. Hili pia ni jambo jingine la kazi ya Yesu ya kutukomboa. Kama inavyosema “Unatambua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba alikuwa tajiri, lakini kwa niaba yetu amekuwa maskini, ili kwa njia ya umaskini wake tuweze kuwa tajiri” (2 Cor 8:9).
Simeoni alikuwa mtu mwenye haki na aliyejitoa. Roho Mtakatifu alikuwa juu yake na alimpa ufunuo wa kinabii. Alikuwa akitarajia faraja ya Isaeli, ambayo ni alama ya rafaja ya Israeli ambayo wanapokea Waisraeli kwa njia ya Masiha. Anna kwa upande mwingine alikuwa nabii. Baada ya kumuona mtoto Yesu, aliongelea kuhusu Yesu kwao wote waliokuwa wakitarajia ukombozi ambao Masiha angeleta. Siku hii ya leo tukumbuke pia kujitolea kwetu kwa Bwana kwa njia ya Ubatizo. Tujitoe wenyewe kwa Bwana na ufalme wake bila kuwa na mioyo iliogawanyika.
Sala:
Bwana nilizaliwa katika hali ya dhambi. Pokea sadaka yangu mwenyewe ya unyenyekevu na naomba unifanye nistahili ufalme wako. Yesu anakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni