Ijumaa, Januari 06, 2023
Ijumaa, Januari 6, 2023
1 Yoh 5:5-6, 8-13;
Zab 147: 12-15, 19-20;
Lk 5:12-16.
HAKUNA ASIYEFAA MBELE YA YESU!
Katika Injili ya leo, Yesu anamponya mtu mmoja mgonjwa wa ukoma. Wakati wa Yesu wenye ukoma walikuwa waki dharauliwa. Sheria ya Wayahudi ilikataza mtu yeyote kumkaribia mwenye ukoma kwa sababu atakuwa najisi. Kivuli tu cha mtu mmoja mwenye ukoma kikipita juu ya Myahudi ilikuwa inachukuliwa kuwa mtu huyo aliyeguswa na kivuli ametiwa unajisi na ibada yake imeharibiwa. Myahudi huyo alipaswa kuoga na kujitakasa mwenyewe kabla ya kuingia hekaluni. Hiyo ilikuwa hali ya wenye ukoma.
Mwenye ukoma katika Injili ya leo alifanya kitu ambacho nichamuhimu sana. Kwasababu ya hali yao haikutegemewa mkoma kama huyu kusogea karibu na mwalimu lakini Yeye aliamini kuwa Yesu angeweza na atamponya ukoma wake.
Yesu alikuwa na huruma na upendo kwa mtu mwenye ukoma. Yeye akamjalia matakwa yake.
Kama soma la kwanza linavyosema yeye amuaminiye mwana wa adamu atapata uzima tele, mkoma alimuamini Yesu na alipata uzima na kuponywa kabisa.
Hali kadhalika hakuna hata mmoja wetu aliyetengwa na upendo na huruma ya Mungu.
Sala:
Mungu Baba yetu, tusaidie tuweze kuwa na huruma kwa wale wote ambao wanaonekana hawafai katika jamii zetu.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni