Alhamisi. 18 Aprili. 2024

Tafakari

Jumapili, Januari 08, 2023

Januari 8, 2023

Sherehe ya Tokeo la Bwana (Epifania)

Isa 60: 1-6;
Zab 72: 1-2, 7-8, 10-13;
Efe 3: 2-3, 5-6;
Mt 2: 1-12.


ZAWADI KWA DUNIA NZIMA!


Katika somo la kwanza, katika ono lake la kinabii, Isaya anaona ujio wa Mungu ulimwenguni. Utakuja muda ambapo watu wote wataletwa pamoja mbele ya Bwana na watabarikiwa sana. Utukufu wa Bwana utashuka ulimwenguni na utukufu wake utauzunguka uumbaji wote.

Tukio hili takatifu litalibadilisha jiji la Yerusalemu na wale wote wanaofanya kazi na kuvumilia watapokea mwanga wa uhai.

Katika somo la pili, Paulo anaifumbua siri ambayo Mungu anaitoa kwa utukufu wake watu wote pamoja na wapagani, kuwafanya warithi wa ufalme wake. Anasema “sasa imefunguliwa kuwa wapagani wanashiriki urithi ule ule”. Ukombozi wa ulimwengu, Mungu pia anawapenda wasio Wakristo kwani wao pia ni wapokeaji.

Leo tunasherehekea sherehe ya Tokeo la Bwana. Ni sherehe ya dhihirisho la Bwana wetu kwa watu wa Mataifa. Kulikuwa na mamajusi watatu kutoka mashariki waliokuja kwa Mfalme mpya aliyezaliwa. Mamajusi hawa, watu wa mataifa, ambao hawakuwa katika utajiri wa pamoja wa Waisraeli, walikuwa ni watu waliosoma nyota kwa lengo la kubaini siri na ujumbe wake. Walipokuja katika mahakama ya mfalme, walimuuliza Herode, yuko wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa? Hawakuuliza kama mfalme wa wayahudi amezaliwa? Walikuwa na uhakika kuwa mfalme alikuwa amekwisha zaliwa. Walikuwa tu hawana uhakika wa sehemu yake alipozaliwa, bali juu ya ukweli kwamba amezaliwa walikuwa nao.

Kama tu vile Yeye alivyo jidhihirisha Yeye Mwenyewe kwa wale mamajusi, kila siku Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwetu sisi katika Ekaristi Takatifu. Tunamtukuza Yeye, tunamshukuru na kumfanya yeye afahamike ulimwenguni kote. Basi tujitoe sisi wenyewe kama zawadi na tuunganike naye na kuhubiri:Mungu amejidhihirisha mwenyewe duniani. Yesu anajitoa mwenyewe zawadi kwa dunia nzima.

Sala:
Bwana, niwezeshe niweze kujitoa Mimi mwenyewe kama zawadi kwako.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni