Jumanne. 21 Mei. 2024

Tafakari

Jumanne, Juni 21, 2016

Jumanne, Juni, 21, 2016,
Juma la 12 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Aloisi Gonzaga, Mtawa


2 Fal 19: 9-11, 14-21, 31-36;
Zab 48: 2-4, 10-11;
Mt 7: 6, 12-14.


NJIA NYEMBAMBA!

Katika Injili ya leo Bwana wetu anatuambia, “tuingie kupitia mlango mwembamba, maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo” (Mt 7:13). Tukiangalia maisha yetu kwa ujumla, si kitu zaidi ya msururu wa matokeo ya chaguzi zetu. Kuna wakati tumehuzunikana sana kwa kufanya uchaguzi mbaya na pia kuna wakati tumefurahi sana kwa kufanya uchaguzi au uamuzi sahihi.

Leo Yesu anaongelea kuhusu uchaguzi kati ya njia rahisi na njia iliyongumu. Tuna shawishika kuchagua njia pana na iliyo rahisi na kukwepa njia nyembamba. Lakini katika maisha ya kiuzoefu ya mwanadamu yanatuambia kwamba hakuna njia iliorahisi inayopelekea mafanikio mazuri ya maisha ya mwanadamu. Ukuu/mafanikio mara nyingi ni matokeo ya kazi ngumu. Njia inayoelekea kwenye Ufalme wa Mungu ni nyembamba. Ina mambo yake, inatuhitaji tujitoe, kujikatalia na sadaka. Kutenda dhambi ni rahisi na inaonekana kuwa kawaida kwa mwanadamu, lakini kubaki bila dhambi ni ngumu kwasababu inatutaka kupingana na matamanio yetu. Inatutaka tujikatalie. Na Injili ya Leo inatuambia kwamba ni wachache sana wanaochagua njia nyembamba, walio wengi wanachagua njia iliopana na iliyo rahisi. Ni wachache sana wanao ipokea Injili na kuishi kadiri ya ujumbe wake. Tuombe neema ya Mungu itusaidie tuweze kuchagua njia nyembamba yakutuchukua kwenye ufalme wa Mungu, inatugarimu sisi wakati mwingine kwende kinyume na matakwa ya wengi, unaweza kuchukiwa nakutopendwa lakini kwakuujua ukweli wa Yesu katika Injili, ishi kadiri yake.

Sala: Bwana nioneshe njia itakayo niongoza mimi nifike kwako.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni