Jumatano, Januari 11, 2023
Jumatano, Januari 11, 2023
Juma la 1 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 2: 14-18;
Zab 104: 1-4, 6-9;
Mk 1: 29-39
UTUME WA YESU!
Kwanini Yesu alikuja? Lengo lake lilikuwa nini? Injili ya leo inatoa jibu kuhusu maswali haya. Yesu alikuja kuhubiri kuhusu Yeye mwenyewe kama UKWELI unao ongelewa. Alikuja kama ufunuo kamili wa Mungu wa mbinguni na ni ufunuo wa ukweli wote. Alikuja kujitoa mwenyewe, katika utimilifu wote, na kwa ajili ya watu watu wote. Anaendelea kujitoa kwetu wote kila wakati tunapo msikiliza katika maandiko matakatifu. Neno la uzima la maisha yake.
Kama Kristo alivyotembelea kijiji na kijiji, anatamani pia kutembelea kijiji cha akili na mioyo yetu. Anataka kututafuta wewe na mimi na kuleta si tu maneno ya uzima wa milele, bali yeye mwenyewe. Je, tupo tayari kuongozwa na Yesu? Je tuna mruhusu aongee na sisi katika ufasaha na ukweli wote?
Katika Injili pia tunaona, njia ya utume wa Yesu. Ni sala, kuhubiri Injili, kuponya wagonjwa na kufukuza pepo wabaya. Tunapaswa kufuata njia hii ya Yesu kama sisi ni washiriki wa utume wake na wafuasi wake.
1: Sala – tunaitwa kuchukua muda kuwa pamoja na Mungu wetu. Tenga muda wa sala na masifu. Kama wafuasi, tunaenda kumtafuta Yesu. Si kwa sababu Yesu amepotea, lakini kwa sababu, tunapotea na tunahitaji msaada wake na uongozi wake.
2: Kuhubiri Injili – Kwa watu wachache, tunaweza kuhubiri kirahisi. Lakini mahubiri hayo si kwa maneno tu. Mtakatifu Fransisko wa Asisi aliwaaambia ndugu zake, Hubirini Injili daima katika maisha yako, na ikiwa ni lazima tumia maneno. Kuhubiri kwa matendo ya maisha yetu ni muhimu zaidi, kuliko kwa maneno.
3: Uponyaji na Kuwa huru- Tumeitwa kuwa dawa iliyo tamu kwa watu walio karibu nasi. Tunaweza kujiuliza, mimi si mponyaji maarufu kama wale wa kwenye TV. Yesu haitaji wewe kuwa wao, anataka uwe bega la kupumzikia kwa wale walio katika maumivu, mtoto mwema kwa wazee walio telekezwa katika Nyumba za wazee, mzazi kwa yatima. Kuwa kaka / dada wakuleta maridhiano kwa wale waliofarakana, uponyaji, ukuaji katika jamii, kutoa matumaini na ujasiri kwa wale ambao wanahitaji na kujiona hawafai.
Sala:
Bwana Yesu, nakutafuta wewe nipo wazi unitafute mimi. Nijalie niwe wazi kwa yote ambayo unataka kunifunulia mimi nikupokee wewe kama Injili inayoishi. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
frans kasamya
aminaIngia utoe maoni