Ijumaa. 19 Aprili. 2024

Tafakari

Jumanne, Januari 03, 2023

Januari 3 2023
------------------------------------------------

KUMBUKUMBU YA JINA TAKATIFU LA YESU

Somo la 1: 1 Yn 2:29 – 3:6 Yesu amekuja ili akomeshe dhambi, mtu yeyote anayeishi kama apendavyo Mungu, hatendi dhambi.

Wimbo wa katikati Zab: Zab 98: 3-4 Miisho yote ya Ulimwengu imeuona wokovu wa Mungu wetu.

Injili: Yn1: 29-34 Yohane Mbatizaji anamuonesha Yesu kama Mwanakondoo wa Mungu.
------------------------------------------------


TAZAMA MWANA KONDOO WA MUNGU

Wakristo wamekuwa watoto wa Mungu wamepata nafasi ya kuwa watu katika familia yake (1 Yn2:29-3:2). Wanapaswa kuonesha ufamilia wao kwa kuishi maisha ya haki. Yohane anasema kwamba wale watu ambao wanaendelea kutenda dhambi hawajapata kumwelewa Yesu bado. (1 Yn 3:6). Yohane alikuwa hasemi kwamba Wakristo hawatakaa waingie katika dhambi, bali wasiishi katika hali ya dhambi. Yesu alikufa ili atutoe kutoka katika utumwa wa dhambi.

Katika somo la Injili, Yohane anasema wazi kwamba “Yesu ni Mwanakondooo wa Mungu anaye aondoa dhambi za ulimwengu” (Yn 1:29 rejea. Isa 53:4-7,10-12). Yesu ni chanzo cha wokovu wetu! Hatukombolewi tu kwasababu ya matendo yetu mema (reje. Tit 3:5); tunakombolewa kwa damu ya Kristo!( Rej. Ufu 1:5; 5:9; Rom 5:1) manenno haya yanasemwa daima na Padre pale tunapo hudhuria misa takatifu akiwa ameshikilia Ekaristi takatifu: “Tazama Mwana konddoo wa Mungu na pale tunapo tazama Ekaristi takatifu, hata pale inaposhikwa wakati wa misa ili sisi sote tuone, tunamuona Yesu Mwanakondoo wa sadaka, katika hali ya kuonekana zaidi. Tunaona na macho yetu, mkate. Lakini macho ya Imani, tunaona Mwokozi wetu. Mwana kondoo wa Mungu daima anaendelea kuja kwetu daima kila siku. Yeye ni yote yanayo tuzunguka, akija kwetu katika hali iliyofichwa, akijifunua mwenyewe katika Imani. Je, unamuona yeye? Tutafakari leo juu ya hayo maneno Matakatifu, “Tazama Mwanakondoo wa Mungu”. Tumtafute yeye na kumpata kwa macho yetu ya Imani na kufurahia kuwa karibu naye. “

Kila mmoja katika mwili wa Kristo ana nafasi ya kufanya kama Mt. Paulo katika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho alivyo andika. Tunakula mkate mmoja na kukinywea kikombe kimoja katika Ekaristi na hivyo tunafanywa mwili mmoja. Sisi ni viungo vya Kristo lakini pia sisi ni viungo vya kila mmoja wetu. Hali ya kanisa huoneakana katika hali yetu ya kuwa na vipaji mbali mbali na vipawa vyetu ambavyo vinaleta nguvu katika mwili huu wa Kristo. Tunavyo mruhusu Yesu mwenyewe anyanyuke na sisi tujishushe, picha kamili ya Yesu inakuwa wazi katika ulimwengu huu.

Sala:
Bwana, ninajishikilia katika utukufu wako leo na daima. Ninakutafuta wewe na kukupenda. Ninakuomba unipe macho ya Imani niweze kukuona na kukutambua daima. Nisaidie niweze kujua ni kwa jinsi gani ulivyo karibu daima, Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni