Jumatano, Januari 04, 2023
Jumatano, Januari 4, 2023
Juma kabla ya Epifania
1 Yn 3: 7-10;
Zab 98: 1-9;
Yn 1: 35-42
JE, YESU NI LENGO LA MAISHA YAKO?
Yohane Mbatizaji mwanadamu kama sisi, angeweza kushawishika kujipatia umaarufu aliokuwa akipata uwe kwa ajili yake binafsi. Angeweza kuwa maarufu na kushindwa kuwaonesha watu kwa Yesu. Lakini sicho kilicho fanyika. Kilichofanyika ni kwamba Yohane alitimiza kazi yake vizuri, akiandaa njia na kuwaonesha wengine kwa Yesu muda ulipofika. Wakati Yohane alipowaambia wafuasi wake wawili “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu..” Walianza kumfuata Yesu nakumwacha Yohane. Pengine alijisikia kupoteza wafuasi, lakini kwa upande mwingine alijisikia furaha kuwa alikuwa akitimiza lengo la maisha yake la wakuwaonesha watu kwa Yesu.
Kwahiyo hata sisi pia. Nirahisi kujitafutia umaarufu wenyewe. Ni rahisi kujitafutia hali ya juu na kuwa vigumu kuiachia iondoke. Lakini upendo wa kweli wa Ukristo hauna ubinafsi, haujitafutii mambo yake. Unamwelekea Bwana wetu daima na kuwaongoza wengine kwa Yesu daima. Yohane alituonesha maisha haya ya fadhila, tunaitwa kufanya hivyo. Kwa kuwaonesha wengine kwa Yesu tutaridhika sisi wenyewe na kujazwa Baraka bila kipimo.
Wakati wanafunzi wawili wa Yohane walipoanza kumtafuta Yesu, Yesu alichukuwa jukumu la kuwaalika kwenye kundi lake. Hakuwasubiri ili wapate maelekezo yake kwanza. Bali alikutana nao. Aliwauliza moja ya maswali muhimu katika maisha. “Mnatafuta nini?” walikuwa wakitafuta nini kwa Yesu na walitegemea kupata nini kutoka katika maisha yake? Yesu anatuuliza kila mmoja wetu leo. Unategemea nini na kutafuta nini kutoka Kwake? Yesu anamwalika kila mmoja wetu “Njooni nanyi mtaona?” ya kwamba neno lake ni kweli na ni la milele.
Sala:
Bwana, nisaidie daima niweze kuwaelekeza wote walio katika maisha yangu waje kwako. Nisaidie nijitoe sadaka bila kuwa na ubinafsi wakati wowote. Nisaidie niweze kutambua daima upendo ndio yote kuhusu wewe na kuwasaidia wengine waje kwako na kukufuata wewe. Wakati hili likiwa ni jukumu langu, nisaidie nilitimize na kulishika kwa moyo wote na kwa furaha. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni