Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Januari 05, 2023

Alhamisi, Januari 5, 2023
Juma kabla ya Epifania

1 Yn 3: 11-21;
Zab 100: 1-5;
Yn 1: 43-51

KUWA WATU WASIO NA HILA!

Je, Nathanaeli alikuja kumwamini na kumkiri Yesu kuwa Mwana wa Mungu na Mfalme wa Israeli kwasababu tu Yesu alimwambia alimuona chini ya Mtini? Inaonekana hivyo. Lakini kuna kitu kikubwa zaidi. Kwanza, Nathanaeli alikuwa mtu, mwaminifu, mkweli, na mtu aliye kuwa na mipango ilionyooka katika kumtumainia Mungu. Pili, hali hii ya kuwa mtu aliyekuwa na mipango ilionyooka ilimfanya Nathanaeli kukiri Imani yake juu ya Kristo mara moja. Kivipi? Je ilikuwa ni kitu ambacho Yesu alisema? Ni wazi kwamba ilikuwa ni kitu kikubwa zaidi kilicho muongoza Nathanaeli kukiri Imani yake juu ya Kristo. Ilikuwa ni zawadi ya kiroho ambayo Roho Mtakatifu alimfunulia ndani mwake. Kitu kizuri ni kwamba, Nathanaeli kwa kuwa mtu ambaye asiye ishi maisha ya pande mbili, alimsikiliza Roho Mtakatifu akiongea ndani ya moyo wake na akaongea ukweli huu kwa ujasiri mkubwa na kwa ukweli wote.

Katika maisha yetu tunapaswa kuiga maisha haya ya Nathanaeli. Tunapaswa tuwe wawazi kwa Roho Mtakatifu anayeongea ndani mwetu, na tunapaswa kuwa jasiri kwa ukweli huu uliowekwa ndani ya mioyo yetu ili tuweze kuufunua katika kweli na kwa uaminifu kwa wengine. Kwa kuiga mfano huu, tutaweza kuishi kama vyombo vya Bwana kwa kila tutakaye kutana naye. Tujitolee wenyewe kuwa vyombo vya sauti ya Mungu katika ulimwengu huu kwa kumuiga huyu Mtume.

Sala:
Bwana, natamani kusikia na kufahamu sauti yako ikiongea ndani ya moyo wangu. Nitakavyo kusikia wewe, nisaidie niweze kuwa tayari kukufunua wewe kwa wengine. Yesu, Nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni