Jumanne, Disemba 27, 2022
Desemba 27, 2022
------------------------------------------------
JUMATANO, OKTAVA YA NOELI
Sikuu ya Yohane, mtume na Mwinjili
Somo la 1: 1Yn 1: 1-4 Yohane, akiwawakilisha Mitume, anatuambia kwamba msingi wa kuhubiri kwao ni kwa kitu kile ambacho wameona na kusikia”Neno la uzima”.
Wimbo wa katikati: Zab 96: 1-2,5-6,11-12 Bwana ni Mfalme, dunia ifurahie, bahari ishangilie. Furahieni enyi wenye haki katika Bwana, mpeni utukufu wa jina lake.
Injili Lk 1: 26-38 Yohane anaonesha hali yake yeye na Petro ya kufika kaburi la Yesu asubuhi siku ya pasaka na kukuta kaburi wazi.
------------------------------------------------
NENO ALIFANYIKA MWILI KWA AJILI YETU!
Siku ya leo ni siku ya sikukuu kwa Yohane mtume na Mwinjili. Hakuandika tu injili bali pia waraka tatu na katika hizo barua Yohane anaelezea kwa undani kuhusu kile alicho kielezea katika sura ya kwanza ya Injili kuhusu Neno wa milele, ambaye alikuwako tangu mwazo, akachukuwa mwili. Hapa anaelezea kwamba “kile ambacho kilikuwepo tangu hapo awali..kimefanywa wazi kwetu nasi tumeona” Mwana wa milele wa Baba alichukuwa mwili kama wetu ili sisi tuweze kumuona. Yohane alikuwa shahidi wa hili. Kwa Yohane umwilisho ilikuwa hakika na isiyo kwepeka na yenye kufanya yote upya. Yohane alitoa maisha yake ili kuhubiri habari njema. Alitoa muda wake ili kutafakari mafumbo haya kwa kuruhusu mwenyewe kuona, zaidi, kwamba Mwanadamu aliye tembea naye na kukaa naye alikuwa Mungu na mtu. Huenda ingebaki kuwa tu ni kile alicho kiona lakini alizama zaidi ya yale aliyo yaona. Kidogo kidogo aliweza kufahamu Yesu yupo hai katika maisha yake mwenyewe.
Hata katika ufufuklo ni Yohane aliyemtambua Yesu katika ziwa Galilaya. Wakati ambapo walikuwa hawajakamata kitu chochote alafu yule mtu wasiye mjua na kuwaambia watupe tena jarife baharini, Yohane alikuwa mwelewa wa haraka wa Bwana na kusema kwamba “Ni Bwana”. Hili linatuleza ni kwa jinsi gani Yesu alivyogusa maisha yake. Aliweza kuhisi uwepo wake ingawaje hakuwepo kimwili. Upendo unafahamu mambo yote, hauna mipaka.
Noeli inatuletea ujumbe kwamba Mungu ni upendo. Tuombe neema ya Mungu ili tuweze kumfahamu Yesu, kwani uhusiano kati yetu na Yesu ndicho kinachoweza kufanyika kwetu. Tutoe sala ya shukrani kwa zawadi ya ufahamu wa Yohane wa kuandika maandiko matakatifu, tujaribu kuingia katika akili yake na moyo wake kama alivyokuwa akisali na kutafakari kuhusu maisha ya Kristo.
Sala:
Mungu Baba yetu, umefumbua mafumbo ya neno lako kwa njia ya Yohane mtume. Kwa njia ya sala na tafakari, tunaomba tuweze kuelewa hekima aliyofundisha. Pamoja na Yohane tunaomba tushiriki katika hekima iliyojificha katika mafumbo ya Neno wa milele unayotufunulia katika Ekaristi takatifu daima. Kwa Kila Ekaristi tunaomba daima Mwanao aishi ndani mwetu, kwani yeye ni Bwana Milele na Milele.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni