Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Januari 27, 2017

Ijumaa, Januari 27, 2017,
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa


Ebr 10: 32-39;
Zab 37: 3-6, 23-24, 39-40;
Mk 4: 26-34


MBEGU ZA UFALME WA MUNGU!

Leo Yesu anaelezea habari ya mtu anaye mwaga mbegu zake ardhini. Ikisha oteshwa, anasubiri mpaka itakavyo ota na kukuwa na kutoa mavuno. Haelewe ni kwa jinsi ghani zinavyokuwa, lakini siku ya mavuno ifikakapo anavuna. Yesu pia anaongea kuhusu mbegu ya haradali. Hii ni ndogo sana lakini ina utajiri ndani yake. Hii mbegu pamoja na kwamba ni ndogo sana ina utajiri ndani yake ya kuweza kuwa mti mkubwa, na kuwa chanzo cha chakula kwa ajili ya ndege na sehemu ya kupumzikia ya ndege.

Huu ni ni kukweli unao dhihirisha kwamba Yesu anapenda kumtumia kila mmoja wetu katika kujenga ufalme wake. Tunaweza kujisikia kwamba hatuwezi kufanya mengi sana, na kwamba hatuja pewa vipaji vingi kama wengine, na kwamba hatuwezi kuleta mabadiliko makubwa, lakini hii sio kweli. Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu amepewa vipaji vingi vya ajabu na Mungu ambavyo Mungu anapenda vizae matunda. Anataka alete kutoka ndani mwetu vitu vya utukufu kwa ajili ya Ulimwengu. Tunachopaswa kufanya ni kumruhusu yeye afanye kazi ndani yetu. Kama mbegu, tunapaswa tujiruhusu wenyewe kujiotesha kwenye udongo wa huruma yake kwa njia ya Imani na kujikabidhi kwenye mapenzi yake. Tunapaswa tujimwagilie kwa sala za kila siku na kuruhusu mwanga wa wake utuangazie ili aweze kuvuna matunda apendavyo kutoka ndani yetu na alicho otesha tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Ametufanya sisi kwa lengo la kuleta Ufalme wake ndani yetu. Ni jukumu letu kumruhusu Mungu afanye yote ndani yetu ambayo amepanga katika maisha yetu.

Sala: Bwana, nakupenda na ninakushukuru kwa yote uliotenda katika maisha yangu. Ninakushuru kwa namna ya pekee, kwa yote, ambayo najua utatenda katika maisha yangu. Ninakuomba ili niweze kujikabidhi kwako, ili uweze kunitakasa mimi kwa neema yako, naomba ulete katika maisha yangu matunda mema. Yesu nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni