Jumatano, Novemba 30, 2022
Jumatano, Novemba 30, 2022
Juma la 1 la Majilio
Sikukuu ya Mt. Andrea Mtume,
Rum 10: 9-18;
Zab 19: 2-5 (R. 5);
Mt 4: 18-22.
FUATA NA ONGOZA!
Mt. Andrea anaonekana kuwa mfuasi muwazi. Andrea hana utambulisho kwenye Injili isipokuwa ule wakutoka kwa Yesu. Anajulikana kila mara kama anayemfuata Yesu au anayewaleta wengine kwa Yesu. Ingawaje alikuwa ni mfuasi aliyekuwa na faida nyingi kwa kuwa karibu na Yesu. (Mk 13: 3), alijishusha kabisa kwa unyenyekevu na kuwaleta wengine kwa Yesu bila ya kujijali yeye peke yake tu (Yn 1: 40-42).
Wakati mtume Filipo alivyofuatwa na kundi la Wayunani waliotaka kumuona Yesu. Badala ya kuwaleta moja kwa moja kwa Yesu, Filipo aliwapeleka kwa Andrea (Yn 12:20-22). Filipo alikuwa na uhakika kwamba kama akiwafikisha hawa watu kwa Andrea ana hakika kwamba atawapeleka kwa Yesu moja kwa moja. Alikuwa pia chombo cha kumwakilisha yule kijana kwa Yesu aliyekuwa na samaki na mkate, ambapo baadae Yesu alifanya muujiza wa kuongeza samaki na mikate.
Mt. Andrea anatupa sisi mfano wa Imani kubwa. Kama Mt. Paulo anavyosema katika barua yake kwa Warumi “Imani inakuja kwa kusikia, na tunachosikia kimetoka kwa Yesu” (Rum. 10:17) Mitume walisikia sauti ya Yesu ikiwaita, na wakafuata, wakiwa wakionesha Imani. Kwa Mtume Andrea tunajiona wenyewe na utume wetu. Kumfuata Yesu ni jukumu letu la kwanza na kuwaongoza wengine kwake ni utume wetu.
Sala:
Bwana, ninakushukuru kwa kunijali kila mara katika maisha yangu. Asante kwa ukamilifu wako wa kunijali katika mahitaji yangu. Ninaomba kila mara nikuamini wewe, katika ukamilifu wako wa kunijali na naomba nijikabidhi katika upendo wako mtakatifu. Yesu nakuamini wewe.
Amina .
Maoni
Ingia utoe maoni