Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Novemba 22, 2022

Jumanne, Novemba 22, 2022
Juma la 34 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Sesilia, Bikira na Mfiadini,

Ufu 14:14-19;
Zab 95:10-13;
Lk 21:5-11


KUJIANDAA KWA MWISHO WA ULIMWENGU!


Vitu vyote vizuri vinafikia mwisho. Vyote vilivyo na mwanzo vina mwisho. Mungu aliweka mwanzo wa Ulimwengu huu, atasababsha pia mwisho wake. Somo la kwanza la leo linatilia mkazo kuhusu nyakati za mwisho, na hasa somo la kwanza kutoka katika kitabu cha ufunuo. Ujumbe kutoka katika kitabu hiki unastusha. Pia Injili ina ujumbe unao fanana, inaelezea jinsi ya muda wa kutisha ulivyo karibu. Lakini Yesu anamalizia kwa namna tofauti akielekeza kwamba tusimame imara, tusitishwe na wala tusidanganywe na mafundisho tofauti. Kitu cha muhimu sio kitatokea nini bali ni jinsi ghani tunapokea kwa Imani na kuenenda kwa Imani kwa yanayo tokea? Haijalishi ni lini au ni namna ghani ulimwengu utakavyo ishia, tunatambua sisi wote karibuni au baadae, kila mtu atakumbana na mwisho wake (kifo) ambapo kila mmoja anamapaswa kutoa hesabu ya maisha yake. Je, tumeishi kwa Imani? Kama ndio, tutakuwa tayari kwa ujio wa Bwana wetu, vichwa vyetu vikiwa juu!

Sala:
Bwana, nashukuru kwa kunikumbusha mimi jinsi ya kujiandaa kukutana na wewe. Nijalie neema niweze kuishi wakati wangu kwa mafanikio.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni