Jumatatu, Novemba 21, 2022
Jumatatu, Novemba 21, 2022
Juma la 34 la Mwaka
Kumbukumbu ya kutolewa Bikira Maria Hekaluni
Zek 2:14-17;
Lk 1:46-55;
Mt 12:46-50
SADAKA ILIYO KAMILI!
Leo Kanisa linakumbuka siku ya kutolewa Bikira Maria Hekaluni katika Hekalu la Yerusalemu. Inawezekana huenda manabii hawa watakatifu simeoni na Anna. Walioshuhudia kutolewa kwa Yesu hekaluni, kama inavyo oneshwa katika sura ya pili ya Injili ya Luka, huenda walimfahamu mama wa Yesu akiwa msichana mdogo hekaluni na kutambua ukweli wa utakatifu wake wa pekee. Kujiweka Bikira Maria wakfu kwa Mungu kunaeleza sifa zote za sadaka ilio kamili: alikuwa tayari, mkarimu, mwenye furaha, hakujuta, na hakujibakiza. Ni kwa jinsi ghani ilimpendeza Mungu! Tunamuomba Mungu kujiweka kwetu wakfu kwake, kuweze kuwa chini ya ulinzi wa Mama Maria tukisaidiwa na maombi yake yenye nguvu, na nafasi yake ya pekee alio nayo kwa Mungu.
Katika somo la kwanza Mungu anatuambia tufurahi kwasababu anakuja kukaa kati yetu. Katika Agano la Kale “binti Sayuni”, ilikuwa ni kati ya majina mengi ya watu wa Mungu. Tunapo litumia leo katika Liturjia zetu tuna maanisha Kanisa, lakini pia tuna maanisha Mama wa Mungu aliyekuwa karibu na Yesu na yeye ni mfano kamili wa kutekeleza mapenzi ya Mungu. Katika Injili ya leo, tunasikia Mama mmoja akimwambia Yesu “Heri tumbo lililokuzaa,” na Yesu anatumia muda huo kuelezea thamani ya kuyafanya mapenzi ya Mungu. Nini maana ya “kufanya” mapenzi ya yake? Kufanya mapenzi mapenzi nikufanya kile unacho kifahamu kinaendana na mapenzi yake. Neno lake linapaswa kuongoza katika mioyo yetu. La pili, yeye familia yake ipo ulimwenguni mwote (familia ya Utatu katika Umoja). Wakristo wanapata kuwa watoto katika familia hii, sio kwa kuzaliwa, bali kwakufanya mapenzi ya Mungu. La tatu, kufanya mapenzi ya Mungu inatupasa kuwa na uhusiano mzuri naye. Kitu kinacho haribu uhusiano wetu na Mungu ni dhambi. Ili kufufua uhusiano wetu na Mungu lazima kukubali makosa yetu na kuachana nayo. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuungama dhambi zetu na kutubu. Mungu yupo tayari daima kutupokea ili tufanye mapenzi yake, lakini tupo tayari kufanya mapenzi yake na kurudi katika kundi lake?
Sala:
Ee Maria, tufundishe jinsi ya kujitoa kama sadaka ilio hai kwa Mungu.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni