Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Novemba 04, 2022

Ijumaa, Novemba 4, 2022
Juma la 31 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Karoli Borromeo, Askofu

Fpl 3:17 - 4:1
Zab 121:1-5
Lk 16:1-8


RAIA WA MBINGUNI

Katika Masomo ya leo, Mt. Paulo anawaambia Kanisa la Wafilipi na sisi leo pia, ni sifa zipi za raia Mkristo anayeishi katika Ulimwengu huu. Kwanza, wanapaswa kuiga sheria njema za Kikristo (mstari 17), pili, waachane na mambo ya ulimwengu yalio adui wa msalaba (mstari 18-19) na tatu, wakumbuke kwamba uraia wao halisi upo mbinguni (mstari 19). Kwa hayo yatawafanya wawe raia wema hapa duaniani (Mstari20-21). Paulo, bila kuwa na hofu anawaambia Wafilipi waige na wafuate mfano wake wa kuwa na imani, na hivyo hawata yumbishwa na kupoteza njia yao na wale wapotoshaji. Maelekezo ya Paulo jinsi ya kuwa raia wa mbinguni yanatufaa nasi leo hii katika maisha yetu. Sisi pia, tunaweza kuiga na kuishi namna yake ya kujikatalia na kuamini na furaha ya kujitoa sadaka. Ifikie mahali tuweze kusema kama Paulo tena kwa ujasiri kwamba watu waige Imani yetu tulio nayo kwa Kristo.

Sala:
Baba wa mbinguni, tusaidie kila wakati tutambue kuwa sisi ni raia wa mbunguni na tuishi kwa mfano wa Kristo na mifano mingine katika kanisa lako.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni