Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Januari 26, 2017

Alhamisi, Januari 26, 2017,
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Watakatifu Timotheo na Tito(Maaskofu)

2 Tim 1: 1-8 au Tit 1: 1-5;
Zab 96: 1-3, 7-8, 10;
Lk 10: 1-9.


WAJUMBE WA AMANI

Leo tunaangalia juu ya wazee wetu wa Imani na jinsi walivyo weka Injili katika matendo yao baada ya ufufuko wa Yesu. Hawa wanaume na wanawake ni wa kizazi cha pili: wafuasi wa wafuasi na walikuwa wakitumwa mara kwa mara wakiwa wawili wawili kuhubiri kwa uwepo wao. Kwa njia ya kutembelea na kusafiri inaonyesha kwamba ufalme wa haki na Amani ulikuwa tayari Ulimwenguni.

Ujumbe kutoka katika barua kwa Timotheo, Paulo anaelezea mapendo yake makubwa kwa Timotheo, na wenzake katika utume, na hamu yake kubwa ya kumuona. Anamshukuru Mungu kwa Imani ya Timotheo alioonesha kwa mama yake Myahudi na bibi yake Loisi. Wakati huo huo anamkumbusha Timotheo kuhusu zawadi aliopokea wakati Paulo alivyo mwekea mikono juu yake. Zawadi anayosema Paulo, ilikuwa sio ya woga bali yenye nguvu, upendo na ujasiri na kuleta ujasiri wote wakuhubiri Injili hata wakati, wa kipindi cha Paulo, kuonewa na kuteswa. Katika somo la kuchagua la pili, kutoka katika barua ya Paulo kwa Tito, Paulo anawakumbusha wamisionari wenzake juu ya kazi ya mtume. Ni “kuwaleta wote ambao Mungu amewachagua kwenye Imani na akili ya kweli inayo ongoza kwenye dini ya kweli”.

Katika somo la Injili linaongelea kuhusu maelekezo anayotoa Yesu kwa wale Wafuasi 72 anavyowatuma kwenda kwa utume kufanya kazi ile ile aliokuwa akifanya yeye mwenyewe. Maneno yake ya ufunguzi ni kweli kama ilivyokuwa katika kipindi cha Timotheo na Tito: “mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache; hivyo muombeni Bwana wa mavuno apelike wafanya kazi katika shamba lake.” Ujumbe wao ulipaswa kuwa wenye kuponya. Sio tuu uponyaji wa mwili tu, bali uponyaji wa kila aina unaofanya mahusiano na maisha ya watu yalete Amani. Kwa kufanya hivi walileta uwepo wa ufalme wa Mungu kwa watu walio watembelea. Ni upendo na uwezo wakuishi kwa pamoja kwa kujaliana na kusaidiana vinaonesha uwepo wa Ufalme wa Mungu katika maisha yetu. Haya ndio Timotheo na Tito walijitolea kufanya. Sisi-hata tungekuwa na cheo ghani katika jamii ya Kikristo-tunaitwa kufanya hayo hayo.

Sala: Bwana, ninaomba niwe mjumbe wako wa Amani na uponyaji. Ninaomba nijifunze kutegemea nguvu zako na kuishi maisha nikijikabidhi katika utume wako. Yesu nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni