Ijumaa, Oktoba 14, 2022
Ijumaa, Oktoba 14, 2022
Juma la 28 la Mwaka wa Kanisa
Ef 1:11-14;
Zab 32:1-2, 4-5, 12-13;
Lk 12:1-7
KUTANGAZA INJILI BILA WOGA!
Je, inakusumbua kuhusu wengine wana waza nini juu yako? Kwa namna unavyo vaa? Kwa namna unavyosema? Je, unashindwa kufanya kitu flani au kutokufanya kwasababu mtu flani atafikiri je? Hii ndio hofu ya mwanadamu na hii sio hofu sahihi. Hofu sahihi ni hofu ya Mungu, kuhusu anachofikiri na anacho tuamuru, na nini anacho tegemea. Lakini sio kwa hofu kama ya mtu anaye adhibu. Hofu ya mwamini ni heshima kwa Mungu. Hofu hii ni msukumo wetu wakujikabidhi kwa Muumbaji wa ulimwengu. Ambaye ni Mungu.
Katika Injili ni mwaliko wa kuwa bila hofu na hasa wakati wa majaribu na mateso. Mkristo hapaswi kuwa na hofu anavyo hubiri Injili ya upendo, ndio, hata katika mapaa ya nyumbani. Ili kuhubiri huku kuwe na matunda kamili, Mungu amesia ndani mwetu na kututia mafuta kwa Roho Mtakatifu (Ef 1:13; 2Kor 1:21) kama kusimikwa kwetu kwanza kwa ajili ya safari ya wokovu wetu. Hatujapokea roho wa utumwa wa kutupeleka kwenye hofu, bali Roho wa Mwana ambaye kwa njia yake tunalia ‘Abba Baba” (Warumi 8:15). Kwa ajili ya kuhubiri kusiko na hofu, na sio kuanguka kwenye hofu na ni vizuri kwamba tukuwe katika Roho Mtakatifu.
Sala:
Bwana, tusaidie tuweze kutenda kwa kadiri wa Roho asiye na hofu, ambaye umetuita kuhubiri katika Injili.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni