Jumamosi. 27 Aprili. 2024

Tafakari

Ijumaa, Septemba 23, 2022

Ijumaa, Septemba 23, 2022 

Juma la 25 la Mwaka


Kumbukumbu ya Mt. Padre Pio wa Pietrelcina, Mkapuchini.

Muh 3: 1-11
Zab 143: 1-4 
Lk 9: 18-22


KRISTO NI NANI KWANGU?

Katika Injili tunamuona Yesu akiwauliza wanafunzi wake maswali mawili. “watu wanasema mimi ni nani? na “nyie mnasema mimi ni nani?” Yeye mwenyewe alijitambua ni nani. Kwahiyo, Yesu anauliza maswali kama mpango wake wakuendelea kujifunua kwa wanafunzi. Alitaka wanafunzi wake wamtambue yeye, ametoka wapi na kwanini amekuja. Swali la Yesu pekee lili hitaji jibu la mtu binafsi kutoka kwa Wanafunzi wake. Hata sisi leo Yesu ana tuuliza swali hilo hilo: ‘wewe unasema Yesu ni nani?’. 

Leo tuna adhimisha kumbukumbu ya Mtakatifu Pio wa Pietrelcina maarufu kama Padre Pio. Huyu ni mtakatifu wa kipindi chetu tuu, huyu alimtambua Yesu ni nani na aliishi kadiri ya mapenzi yake. Alimuishi Yesu mpaka akafanana na Yesu, Yesu mwenyewe alimzawadia zawadi ya madonda yake katika mwili wake. Huyu alikuwa mnyenyekevu kweli hata pale alipo ambiwa aache kutoa baadhi ya huduma ili Kanisa liweze kuona ukweli katika yote yaliyo tukia kwake. Hii ni kwasababu Kanisa linatambua wazi kwamba yule muovu aweza pia kutumia mtu kuharibu Imani. Moja ya sifa za Roho wa Mungu aliye ndani ya mtu ni utii na unyenyekevu, Padre Pio alitii na kwa unyenyekevu hadi Kanisa likamrusu tena kuendelea kutoa huduma kama kawaida. Padre Pio anajulikana sana kwa muda wake mwingi alioutumia ili kutoa sakramenti ya Upatanisho. Aliungamisha watu kwa muda mrefu sana, na kwa kadiri ya baadhi ya maandishi yanasema kwamba, Kristo alimpa hata uwezo wakuweza kumkumbusha mtu aliyesahau kutaja dhambi yake au aliyeficha dhambi yake wakati wa maungamo. 

Mfano mmoja wapo ni mama mmoja aliungama, akasahau kutaja dhambi zote, padre Pio alimwambia arudi nyumbani, na alivyorudi wakati akichukua ndoo ili kuchota maji kwenye kisima, na tazama aliona sura ya mtoto wake mchanga ndani ya kisima aliyemtoa miaka mingi angali mimba. Yapo mengi yaliotukia wakati wake na hatuwezi kuandika yote, ni Mtakatifu aliyejua ukuu wa huruma ya Mungu. Ndio maana kwa kipindi hiki cha mwaka wa jubilee ya huruma ya Mungu, Baba Mtakatifu Fransisko, aliomba mwili wa Padre Pio pamoja na Mwili wa Mt. Leopold Mandic ipelekwe Vatican watu waweze kuiutazama, kuenzi mchango wao wa kutambua ukuu wa huruma ya Mungu, uliowagusa wakaweza kuungamisha kwa muda mrefu. Mtakatifu huyu aliweza kumfahamu Yesu kwa moyo kabisa na akamfuata kwa moyo. Kwa muda mrefu tumekuwa tukimfuata Kristo. Je, tumeshamtambua Yesu, mimi binafsi? Kristo ni nani kwangu? 

Sala:
Bwana, nisaidie niweze kuku fahamu wewe kwa karibu kabisa na kukuamini.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni