Jumanne. 23 Aprili. 2024

Tafakari

Ijumaa, Septemba 16, 2022

Ijumaa, Septemba 16, 2022 
Juma la 24 la Mwaka

Kumbukumbu ya Watakatifu Kornelio, Papa, na Sipriano, Askofu, Wafiadini 

1 Kor 15: 12-20
Zab 16: 1, 6-8, 15
Lk 8: 1-3


MCHANGO WANGU KATIKA UTUME WA BWANA!

Luka anatuambia kuhusu kazi kubwa waliofanya idadi kubwa ya wanawake katika kutegemeza utume wa Bwana wetu na Wafuasi. Pamoja na tofauti zao kati ya wanawake, lakini inaonekana wote walikuwa na kitu cha pamoja kwamba: Yesu amewaponya kimiujiza kwasababu ambayo hakuna jibu sahihi kutoka kwa Mwanadamu. Katika hali ya kufikirika, kundi lililo fuatana na Yesu lilitoa ushahidi na kumtambulisha Yesu kama Kristo Masiha. Wanawake hawa hawakuwa watu wasiojitambua waliofuata tu, walikuwa watu waliokuwa hai katika kutangaza Injili ya Ufalme wa Mungu. Wakati Yesu alivyo watuma wale kumi na wawili (Lk 9: 1-6) na wale sabini na mbili (Lk 10: 1-12). Aliwaambia wasichukue chochote. Hii ni kwasababu walikuwa wafanye utume kwa wale waliowafuata, ambao kati yao waliishi miongoni mwao. Tunapaswa tuwe tunafanya walichofanya wanawake hawa. Walimpenda Yesu sana, walimtumikia yeye na wafuasi wake kwa vile walivyokuwa navyo. 

Je unadhani Yesu alihitaji msaada wao? Hapana. je, alihitaji chakula chao? Hapana. Kama Yesu angependa angeweza kuchukua tu kipande cha mkate katika mkoba, na pale watakapo hisi njaa yeye na wafuasi wake Yesu angeiongeza hata kuwa kikapu kilicho jaa. Kwanini hakufanya hivyo? Hii ni kwasababu kama kuna kitu anachopenda Yesu zaidi kuliko kuwalisha watu, ni wakati watu wanampa yeye kwasababu wanampenda. Hahitaji yote hayo, bali anapenda kupokea. Inampa furaha kubwa tukimpenda. Yesu hajapungukiwa chochote, tukimpenda na kumtumikia ni faida kwetu sisi kwamba tunampendeza Bwana, nasi tunajipatia Baraka kwa ajili ya roho zetu. Tunajua kwamba sala zetu hazi muongezei Mungu kitu, ila za faa kwa ajili ya wokovu wetu. Tumtumikie Mungu kwa uchaji katika wema na kweli ili tujipatie utakatifu wa roho zetu.

Sala:
Bwana, nijalie moyo wa ukarimu.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni