Jumatatu. 16 Septemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Januari 23, 2017

Jumatatu, Januari 23, 2017.
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa

Siku ya sala kuombea kuwa na sheria ya kulinda watoto ambao hawajazaliwa

Ebr 9: 15, 24-28;
Zab 98: 1-6;
Mk 3: 22-30.


KUACHA DHAMBI

Leo sehemu ya Injili inatufunulia kuwa kuna dhambi Fulani, dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ambayo haita samehewa. Hii dhambi ni ipi? Kwanini hai sameheki? Hii ni hali ambayo mtu anatenda dhambi ya mauti na kushindwa kujisikia hali ya kutotubu na kujiona kama hana kosa au kukataa huruma ya Mungu inayo muita kufanya toba ya kweli. Hali hii yakuto jisikia kwamba ametenda dhambi inafunga mlango wakuruhusu huruma ya Mungu. Lakini pia itambulike kwamba, wakati roho ya mtu inapo badilika na kuonyesha kutubu kwasababu ya dhambi, Mungu anamkaribisha mara moja mtu huyo kwa mikono miwili. Mungu hawezi kamwe kumkataa mtu yeyote anaye kwenda kwake kumwomba msamaha kwa moyo mnyofu.

Tutafakari juu ya huruma ya Mungu isio na kikomo, na kutafakari juu ya jukumu letu la kujinyenyekeza mbele za Mungu tunapokosa. Tutimize jukumu letu kwa moyo wa unyofu na Mungu atatupa huruma yake. Hakuna dhambi iliyo kubwa kwa Mungu mtu amwendeapo Mungu kwa moyo mnyofu.

Sala: Bwana, Yesu Kristo, mwana wa Mungu aliye hai, nihurumie mimi mdhambi. Ninakiri dhambi zangu na ninaomba unisamehe. Nisaidie Bwana wangu, nitazame ndani mwangu na nijisikie huzuni kwa dhambi zangu na kujikabidhi katika huruma yako ya Kimungu. Ninakushukuru kwa upendo wako mkamilifu kwangu na kwa wote. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Sala maalumu kwa watoto ambao hawajazaliwa: Yesu, mwanzo na mpenda uhai. Tunakuomba uamshe ndani yetu heshima ya kuhesimu uhai wa watoto ambao hawajazaliwa, amsha ndani mwetu uwezo wakutambua matunda ya tumbo la uzazi sehemu ya muujiza mkubwa wa uumbaji wa Mungu, fungua mioyo yetu tuweze kumkaribisha kila mtoto anayepata uhai. Bariki familia zote, takasa muunganiko wa wanandoa, leta matunda kwa upendo wao. Simamia kwa roho wako chaguzi za mikutano ya wabunge wanaopitisha sheria, ili watu na taifa waweze kutambua utakatifu na asili ya uhai, wa kila maisha ya mwanadamu. Simamia kazi za Wanasayansi na madaktari, ili kwa kila kitu kiweze kuwa ni kwa ajili ya kulinda uhai na ukuwaji wa mwanadamu, bila kukandamiza yeyote na kumnyima haki ya kuishi. Wape mbinu viongozi na wana uchumi, waweze kuandaa mazingira mazuri na hali ya kulinda familia, ili daima waweze kuwa na mazingira ya kupokea watoto wapya wanao zaliwa. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni