Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Juni 13, 2022

Jumatatu, Juni 13, 2022.
Juma la 11 la Mwaka


KUMBUKUMBU YA MTAKATIFU ANTONI WA PADUA, PADRE NA MWALIMU WA KANISA


KUUSHINDA UOVU KWA WEMA!


Injili ya leo inaelezea jinsi ya kupita kutoka kwenye haki ya zamani ya Mafarisayo (Mt 5: 20) kwenda kwenye haki mpya ya Ufalme wa Mungu ambayo inapaswa izidi zaidi na kupita haki ya Mafarisayo. (Mt 5: 20). Inaelezea ni jinsi gani ya kupanda mlima na kwenda kwenye zile heri nane, ambapo Yesu alitangaza sheria mpya ya Upendo. Kilele chake kinaelezewa katika mstari mmoja tuu, “kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa Mbinguni alivyo mkamilifu” (Mt 5: 48)


Kisasi kinadai “jicho kwa jicho, jino kwa jino”. Yesu anafundisha tukitendewa ovu turudishe wema, tukifanya kinyume chake uovu utaibuka na kutawala na hatutajua nini cha kufanya zaidi. Kuwa waaminifu kwa mafundisho ya Yesu, Paulo anaandika kwenye barua yake kwa Warumi “usilipe ovu kwa ovu, badala yake nuiya kuwatendea watu wote mema”. (Rum 12: 17-21). Njia nzuri ya kukabiliana na uovu, nikumwachia Mungu atawale mwenyewe!


Pengine tujiulize sisi wenyewe, hivi nilisha wakwa na hasira kubwa ndani mwangu na nikatamani kulipa kisasi cha “jicho kwa jicho, jino kwa jino”? Nilifanya nini ili kukishinda? Je, maisha katika familia zetu, jumuiya zetu za kitawa, au popote ninapokaa, yanalijenga kanisa na sisi wenyewe katika hali ya upendo ambao Yesu anaeleza leo katika Injili? Je mimi sio mwanzilishi wa fujo na migogoro katika jumuiya au familia yangu? Je, furaha yangu inapatakana pale ninapo waona ndugu au jamaa hawana Amani? Je, ninafurahi ninapoona wenzangu wanafurahi? Au ninatafuta mbinu za kuzima Amani na furaha yao? Je, umekuwa chanzo chakuleta mashindano pale pasipo hitaji mashindo, nakuvuruga upendo na Amani iliyokuwepo? Haya ni maswali ambayo sisi wenyewe tunaweza tusitambue kama tumeyatenda katika hali zetu za maisha kama tutayaangalia kwa haraka haraka bila kutafakari na kujitafiti. Amani inaletwa na sisi wenyewe katika mazingira yetu, Amani na upendo iwe ndio wimbo wa matendo yetu katika maisha yetu. Kujikubali na kuwapokea wengine kwa furaha bila kisasi ni kujenga ufalme wa Mungu kati yetu.


Sala:
Bwana, nisaidie niweze kuiga huruma yako na hali yako ya kusamehe. Nisaidie niweze kuwasamehe wale walio niumiza mimi na nisaidie niweze kuwapenda. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni