Jumanne, Aprili 19, 2022
Jumanne, Aprili 19, 2022,
Oktava ya Pasaka
Mdo 2:36-41
Zab 33:4-5,18-20,22
Yn 20:11-18.
UFUFUKO: WITO WA KUKUWA KATIKA MAHUSIANO NA YESU!
Leo Maria Magdalena anarudi Kaburini baada ya Simoni Petro na Yohane wameshaondoka. Akili ya ufufuko inaonekana haijaingia katika akili yake, ingawaje yeye mwenyewe alikuwa amefufuka katika kaburi katika kufungwa na pepo saba (Lk 8:2). Baada ya kuona kaburi li wazi anabubujika machozi. Uwepo wa malaika haukumuogopesha, kwasababu alikuwa na huzuni kubwa kwasababu ya kupotelewa na mkombozi wa roho yake. Yesu anamtokea ghafla katika huzuni yake na kwa furaha, anasema “Rabi!” Mwalimu!. Yesu anamwambia asimshike.
Huu ulikuwa ni wakati ambao Maria alikuwa na hisia. Alikuwepo alipokuwa akitazama msalaba. Alimfahamu Yesu vizuri na alimpenda sana. Alimtazama akifa na ghafla sasa anamtamzama akiwa amefufuka amesimama mbele yake. Ni wazi kwamba alipatwa na furaha kubwa. Yesu hakuwa mkali kwa Maria kwa kumwambia kwamba asimshike. Alikuwa anampa ushauri mzuri na muelekeo wa safari ya maisha yake ya kiroho na Yesu. Alikuwa anamwambia kwa hakika kwamba, hali yetu sasa inabadilika, na kuwa katika hali ya ndani zaidi. Alimwambia usinishike kwasababu ‘hajapaa kwenda kwa Baba bado’.
Kwa wakati huo uhusiano wa Maria ulikuwa katika ngazi ya kibinadamu. Alipata muda wa kuwa na Yesu, kuwa karibu na Yesu na kumsikiliza, na alimpenda kwa moyo wote wa kibinadamu. Lakini Yesu alipenda yeye na sisi wote, tumpende sasa katika ngazi ya Kimungu. Akiwa katika kiti chake cha enzi Mbinguni anaweza sasa kuingia katika mioyo yetu. Anaweza kuingia ndani ya moyo wa Maria na sisi wote. Anaweza kuishi ndani yetu nasi ndani yake. Na yeye kuwa mmoja pamoja nasi.
Kwa kuacha ngazi ya upendo wa kibinadamu tu na Yesu, Maria aliweza sasa kumpenda katika ngazi ya juu ambayo asingeweza kama alikuwa katika ngazi ya Kibinadamu. Huu ni muunganiko wa Kimungu, ambao kila mmoja wetu anaitwa. Yesu sasa ameshafufuka na sasa tunaweza kushiriki matunda ya ufufuko wake. Sisi, na Maria, tunaweza sasa kumuweka ndani ya mioyo yetu, kwasababu ndiye anaye tutegemeza sisi.
Sala:
Bwana, ninaomba niungane nawe kama wewe ulivyo ungana na mimi. Ninaomba akili, moyo na utashi wangu wote uwe wako. Ninaomba uje uishi ndani ya moyo wangu nami niishi ndani ya moyo wako. Nayatoa maisha yangu kwako, Bwana mpendwa, ninakuomba nikupe yote niliyo nayo na jinsi nilivyo. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni