Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Aprili 17, 2022

Jumapili, Aprili 17, 2022.
Jumapili ya Pasaka

JUMAPILI YA PASAKA

Mdo 10: 34, 37-43
Zab118: 1-2,15-17,22-24
Kol 3: 1-4 or 1Cor 5: 6-8
Yn 20: 1-9


ALLELUIA! YESU AMEFUFUKA KWELI KWELI!

Kwaresima imeisha sasa ni kipindi cha kuadhimisha furaha kuu ya Pasaka! Ulimwengu unafurahia ushindi wa Kristo juu ya dhambi na mauti. Mungu kwa upendo wake kamili na hekima yake, aliishinda dhambi na matokeo ya dhambi(mauti) na kutumia kama njia ya wokovu wa ulimwengu. Kwa kuruhusu dhambi za dunia zimsulubishe na kuteswa na kufanya mateso hayo na dhambi hiyo kuwa kielelezo cha kuleta ukombozi. Yesu aliiangamiza dhambi kwa kuangamiza matokeo ya dhambi ambayo ni mauti. Mauti imepotezwa kwa ufufuko. Ufufuko wa Yesu unaondoa matokeo yote ya dhambi kwao wote wanaojikita kwake.

Kama mateso makali ya Yesu, Mwana wa Mungu, yanaweza kubadilika na kuwa tukio kubwa katika historia ya maisha ya Mwanadamu, ndivyo, mateso yako mwenyewe mizigo yako, hata dhambi zako, zinaweza kuwa chanzo cha furaha yako kubwa kama utamruhusu Mungu ayabadilishe kwenda kwenye ufufuko.

Pasaka maana yake ni hakuna chochote kinacho weza kutuweka mbali na furaha ambayo Mungu anataka kutupatia. Tambua kwamba Mungu anapenda ufurahie furaha ya Pasaka katika maisha yako. Muache yeye akujaze na furaha kuu ambayo ni ufufuko pekee unaweza kuleta. Mungu anataka Pasaka ianze sasa katika maisha yako.!

Katika Injili maneno ya Petro yanachanganyika na majuto ya kumwangusha Yesu. Alisema kwamba atakufa kwa ajili yake, lakini akakimbia. Sasa, Yesu ni mzima! Wala hakuna hukumu. Yesu ametupatanisha naye, tumekaa naye katika mkono wa kuume wa Mungu. Tupo huru kutoka katika sheria ya dhambi na mauti. Tumesamehewa. Maneno tunayosikia kutoka katika maneno ya Petro kama yalivyo andikwa kwenye kitabu cha matendo ya Mitume, yanatikisa kwa furaha yote, nguvu na ujasiri kwamba Yesu, ambaye tulimshuhudia akihubiri na kuponya, tuliye muona akisulubiwa, sasa tumeona kwamba amefufuka, yupo mzima.

Baba Mtakatifu anasema “Kuwa Mkristo sio kwasababu ya matokeo ya uchaguzi wa sheria za maadili, bali kwasababu ya kukutana na tukio, mtu, ambaye anatoa maana nyingine katika maisha na muelekeo mzuri” maisha haya ya kubadilisha hayajawekwa kwasababu ya wachache, bali ni mwaliko wa wote. Kila Mkristo anaitwa kwenye maisha mapya ya kukutana na Yesu Kristo, au kuacha uwazi ndani ya moyo na kumruhusu aingie ndani akubadilishe. Katika siku hii ya Pasaka tusimame imara tukimuomba atufanye wapya kwa kukutana naye. Tutamani kukutana na wengi ambao hawajaona, lakini wakaamini, kwasababu wamesikia. Tuwe mashahidi wa ufufuko.

Sala:
Bwana, ninakuomba nikufanye wewe ubadilishe kila msalaba katika maisha yangu kwenda kwenye furaha Kuu. Bwana, ninaomba furaha yako ijaze maisha yangu na kunijaza nguvu kwa kila kitu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni