Alhamisi, Januari 27, 2022
Januari 27, 2022
JUMA LA 3 LA MWAKA
Mk 4: 21-25
MWANGA WENU UANGAZE
Leo Yesu anatualika kuwa mwanga. Mwanga unaondoa giza mbele yetu. Anatualika pia tusimame mahali ambapo nasi tutaonekana kama taa. Naamini huu wito wakuwa mwanga una nyanja mbili.
Kwanza kabisa katika hali ya mtu binafsi. Kila mmoja wetu amepokea mwanga, ambao ni Roho wa Mungu aliye ndani mwetu. Mwanga unapoingia sehemu yeyote unaonekana. Vivyo hivyo hata maisha ya kiroho. Tunatambua kujielewa wenyewe zaidi. Kila kilichofichwa hutoka kwenye mwanga kama Yesu anavyosema katika mstari wa 22. Hili pia linabeba pia muonekana wa dhambi zetu. Ni kazi ya Roho wa Mungu kuvumbua dhambi na kuturudisha (ref. Yn 16:8-11). Tunachopata kuona ni kile kilichokuwa ndani yetu muda wote, ambacho kilikuwa hakionekana kwasababu hakukuwa na mwanga wa kutosha. Sasa Roho Mtakatifu anatuwezesha sisi tuweze kutambua kile kisicho chema na chenye maadili mabaya na kutuonesha matokeo yake mbaya. Kwa kusaidiwa na mwanga wa Roho Mtakatifu tunaanza kukuwa na kuelewa kile tulichoitiwa.
Sehemu ya pili ni maisha ya pamoja. Taa inapowekwa kwenye kinara haijiangazii peke yake. Bali nikwa ajili ya wengine. Badala ya kujikita katika kujiweka wema peke yetu tujitahidi pia kuwasaidia wengine. Hili ndilo somo la kwanza linalosisitiza. Tunapaswa kufahamu ni kwa jinsi gani tunapaswa kusaidiana kwa mapendo ili kujenga kazi njema. Hatupaswi kujitenga na wengine kama wengine wanavyofanya, bali tupeane moyo Umoja wetu ni kwa jili ya nini? Tunawezaje kusaidiana kwa mapendo na kuleta kazi njema?
Tafakari leo, juu ya maisha ya ukarimu. Kuna njia nyingi mno jinsi ya kuwa mkarimu kwa mwenzako. Jikite katika maisha ya wema na tenda yale yote anayotaka Mungu ndani mwako.
Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa mkarimu katika mapendo yangu na mwenye huruma juu ya wengine. Roho wa Mungu angaza ndani mwangu, ili niweze kujitambua mimi ni nani, nisaidie mimi niweze kuwasaidia wengine wajitambue ya kwamba wao ni nani katika kweli. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni