Alhamisi, Disemba 30, 2021
Desemba 30, 2021.
------------------------------------------------
ALHAMISI, OKTAVA YA NOELI
Somo la 1: 1 Yn 2:12-17 Yohane anaendelea kutuhubiria sisi tena na kutukumbusha juu ya jukumu letu kama Wakristo, na hasa juu ya sisi kuwa macho kwasababu ya malimwengu.
Wimbo wa Katikati Zab: Ps 95: 7-10 Mbingu na zifurahi nchi na ishangilie. Mwabuduni Bwana hekaluni mwake. Ee Dunia tetemeka mbele za Bwana.
Injili: Lk 2: 36-40 Anna, nabii mwanamke, anasali kwa ujasiri kama Simeoni kwa ajili ya Mkombozi. Wakati alipo muona, na kumpa Mungu shukrani na anaondoka na kwenda kumwambia kila mmoja kuhusu hili.
------------------------------------------------
JIBU LA KUKUMBANA NA KIPINDI CHETU CHA NOELI
Ndugu zangu katika Kristo karibuni kwa adhimisho la Misa takatifu, kikubwa tunachokutana nacho katika masomo yetu ni kuhusu, Kukutana na Mtoto Yesu: Nabii Anna tunayemsikia katika Injili hakufungwa na ya dunia. Yeye baada ya kifo cha mume wake aliyatolea maisha yake yote kwa Mungu. Kupendelea kwake kukaa hekaluni kulimbahatisha kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kukutana na Masiha wa Israeli.
Hii iliwezekana kwa sababu hakuwa mtumwa wa dunia kama somo la kwanza linavyotuambia. Nasi tuepuke kuyapenda ya dunia. Tutafute ya mbingu. Tusipofungwa na tamaa za kidunia na kupania ya mbingu hakika tutakutana na mtoto Yesu, Masiha wetu kama Nabii Ana alivyokutana naye. Tuzoee kusoma maandiko matakatifu, kujitolea kwa ajili ya kanisa na kuwasaidia makuhani na watawa. Tuepuke kukaa maeneo yawezayo kukwaza Imani zetu au za wengine. Namna hii tutaweza kukutana na mtoto Yesu na kumshukuru Mungu kama ilivyotokea kwa Nabii Anna.
Tumuombe Roho Mtakatifu tukisema, Ee Roho Mtakatifu naomba unisadie niandae mazingira ambayo nitaweza kukutana na mtoto Yesu daima.
Maoni
Ingia utoe maoni