Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Disemba 13, 2021

Jumatatu, Desemba 13, 2021,
Juma la 3 la Majilio

Hes 24: 2-7, 15-17;
Zab 24: 4-9;
Mt 21: 23-27


JE UNAKUBALI NGUVU NA MAMLAKA YA YESU?

Injili ya leo inaelezea juu ya mafarakano yanayo tokea kati ya Yesu na viongozi wa dini wa wakati huo, baada ya kuwatoa wafanya biashara nje ya Hekalu (Mt 21:12-13). Mungu-Mwenyezi, katika nafsi ya Yesu Mwanae wa tangu milele yote, alikuwa akifundisha maneno ya uzima. Aliongea kwa nguvu na mamlaka na kila mtu alitambua hilo. Lakini Makuhani na Wakubwa wanaonekana wakipata hasira na wivu juu yake , huku wakimuuliza amepata wapi mamlaka? Hili swali linaonesha ni kwa jinsi ghani hawa viongozi wa dini walivyokuwa mbali na ukweli, walikuwa kipofu kabisa. Hawakufungua moyo kupokea ukweli na wala hawakuwa tayari kufungua moyo na kupokea ukombozi wa Mungu katika maisha yao. Na badala yake walisongwa na ubinafsi, majivuno na wifu. Waliogopa kama watakubali kwamba Yohane Mbatizaji na Yesu, utume wao umetoka Mbinguni, watapoteza umaarufu wao juu ya watu na watapoteza mamlaka yao juu ya watu.

Sisi wote tuna uongozi katika hali flani. Hata mazungumzo kati ya watu wawili, kila mtu anamamlaka flani. Kama ulikuwa kwenye hilo hekalu wakati Yesu anaongea, ungejibu nini au ungefanya nini? Je, ungemkataa? Je, ungetamani kumsikiliza zaidi? Je, utakasirishwa nae au kuwa na wivu naye? Je, utatambua nguvu yake ya Kimungu, upendo, mamlaka nakumtafuta yeye? Sisi pia wakati mwingine katika maisha yetu, tunajidanganya na kukimbia ukweli, tunataka tutawale kila kitu bila hata ya Kumruhusu Mungu afanye mabadiliko katika maisha yetu. Leo, tuamue na kukubali kupokea nguvu ya Mungu na tumruhusu yeye awe dereva wa maisha yetu katika furaha na ukamilifu wote.

Sala:
Bwana, nisaidie kuisikia sauti yako ya utakatifu kila mahali. Nisaidie niweze kukutambua wewe kila mahali ninapoenda. Na ninapo kutafuta nisaidie nifurahi kwa kukupata wewe na kukubali yote kwa ujasiri unayosema. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni