Jumamosi, Novemba 27, 2021
Jumamosi, Novemba 27, 2021.
Juma la 34 la Mwaka
Jumamosi, kumbukumbu ya Bikira Maria
Dan 7: 15-27;
Dan 3: 82-87 (R) 59;
Lk 21: 34-36.
KUKUTANA NA MUNGU KATIKA KILA HALI YA MWANADAMU
Leo ni siku ya mwisho katika mwaka wa Liturjia ya mwaka huu. Kesho tunaanza kipindi cha majilio. Mara nyingi Kanisa linaelekeza mambo ya mwisho na mwisho wa maisha yetu hapa duniani. Ni mwaliko kwa waamini kuwa tayari kwa ajili ya mwisho wa ulimwengu. Somo la kwanza linaangalia ni kwa jinsi ghani Watakatifu wa Mungu watakavyo pambana na magumu na changamoto za mwisho wa nyakati, wakati Injili ikituambia kwamba mwisho wa nyakati upo kati yetu kila wakati.
Nabii Danieli anaona ndoto juu ya wanyama wanne. Danieli aliogopeshwa sana na maono haya. Lakini mwishoni anatambua kwamba hakuna mnyama ambaye anaweza kuishi milele.bali utukufu wa mwisho unapewa kwa watakatifu wa Mungu.
Madhulumu kutoka kila mahali haina maana tumeacha neema ya Mungu. Mapingano hayo na ufalme wa Mungu yataendelea mpaka mwisho wa nyakati. Mtakatifu Yohane wa Msalaba alisema kuna maadui watatu ambao tutakutana nao wakati tukisonga mbele kwenda kwenye ukamilifu: shetani, dunia na mwili wetu. Maisha ya mwanadamu yanapaswa kuishia na kuona uso wa Mungu. Na hili ndilo linalopaswa kuwa lengo letu. Hivyo kila mmoja wetu lazima akumbane na adui mmoja wapo katika safari yake.
Yesu anatuambia kwamba tunapaswa kuwa makini. Muda mwingi nguvu zetu zinaishia katika hofu. Kwasababu hatuwezi kutabiri kuhusu wakati ujao tunaishi kuwaza mambo mengi na yasio tusaidia kukuwa kiroho. Badala yake tunapaswa kuongozwa na sala kama silaha yetu katika safari yetu ya hapa duniani. Na hili litafanya safari yetu kuwa ya Amani.
Injili inatuambia kuhusu kukutana na Mwana wa Mungu. Kwanini? Kwasababu yeye ni Bwana wetu, rafiki, zaidi ya yote ni Upendo wetu. Wale wote ambao watamshinda adui watasimama mbele ya Mungu na kumsifu bila mwisho na kumtolea yeye sifa. Ni furaha iliojee!
Sala:
Bwana, ninakupenda wewe Bwana na ninatamani kukupenda wewe zaidi ya yote. Nisaidie mimi niweze kusimama imara katika maisha yangu ya Imani. Nisaidie kukaza macho yangu kwako na kujiandaa utakapo kuja. Ninakuomba nijiandae kwa sala na fadhila, wakati nitakapo kutana na uso wako. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni