Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Januari 10, 2017

Jumanne, Januari 10, 2017,
Juma la 1 la Mwaka.

Ebr 2: 5-12;
Zab 8: 2, 5-9;
Mk 1: 21-28.

KUISIKILIZA SAUTI YA MUNGU!

Leo tunamwona Yesu anaanza utume wake kufundisha watu katika sinagogi. Alifundisha kwa mamlaka makubwa zaidi kuliko walimu wao wa kawaida. Alikutana na mtu mwenye pepo mchafu, ambao walianza kumpigia kelele Yesu: "Tuna nini nawe, Je! umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu."
Yesu anaongea kwa mamlaka makubwa si kwamba alitaka, bali ndivyo alivyo. Yeye ni Mungu na wakati anaongea anaongea kwa mamlaka ya Kimungu. Anaongea katika hali kwamba maneno yake yana gusa mioyo ya watu na kutaka mabadiliko. Hata pepo wabaya wanatambua mamlaka ya Yesu.

Hili linapaswa kutualika kila mmoja wetu kutafakari juu ya mamla ya Yesu katika maisha yetu. Yesu anatamani daima kuongea nawe katika moyo wako na kubadili maisha yako awe nawe akiongea katika mamlaka. Tunaomba maneno yake yazame ndani mwetu yabadili maisha yetu.
Hali kadhalika nasi katika maisha yetu ya kiroho, sisi wenyewe nguvu tuliyopewa na Yesu. Sisi ni watoto wa Mungu. Yule mwovu hutujaribu, anajaribu kutuvuruga sisi na vurugu, fujo na uongo. Je! Tuna nguvu ya kutosha kusimama dhidi yake?

Sala: Bwana, nafungua Moyo wangu juu ya sauti yako ya mamlaka yako. Nisaidie mimi nikuruhusu uongee kwa mamlaka na ukweli. Ukiwa unafanya hayo, nisaidie mimi kubadili maisha yangu na kushinda uovu wote kwa njia ya neema yako. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni