Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Disemba 28, 2016

Jumatano, Desemba 28, 2016,
Sikukuu ya Watakatifu Watoto, Martyrs

1 Yoh 1:5 – 2:2;
Zab 124: 1-4, 7-8;
Mt 2: 13-18.

UTAKATIFU WA MAISHA.


Sisi katika nyakati zetu tumeshuhudia mauaji mbali mbali yanayotokana na siasa. Tunaona katika nchi za Syria, Burundi n.k. Jambo hili limekuwepo muda mwingi katika hisotoria ya mwanadamu ya kutafuta nguvu/uongozi kutoka kwa wanyonge. Katika somo la Kutoka tunamuona Farao akitoa amri ya kuuwawa kwa watoto wa kiume wa Wayahudi. Somo la Injili lina mfanano na somo hilo pia. Herodi anaogopa kupoteza mamlaka yake. Hakukuwa na wakumpinga muda ule, bali aliogopa angekuja baadaye.

Katika nyakati zetu mambo kama haya yanatokea katika sehemu mbali mbali. Kati yetu sio wauwaji wakuuwa kwa mantiki ya kutoa uhai wawengine. Lakini tupo hivyo katika hali, ya kuwauwa wengine kwakuchafua majina yao nakuwasingizia uongo na kuwasema vibaya. Pia kuna uovu wa utoaji wa mimba, kwakujidai kwamba mwili ni wangu naweza kufanya chochote nipendacho. Ambaye anapaswa kutoa upendo na Amani kwa mtoto anajeuka kuwa muuwaji. Jambo hili linapigwa vita na hata dini mbali mbali lakini chakushangaza wengine wanaona utoaji mimba kuwa ni sawa tuu.

Sisi wote tuna jukumu lakufanya. Sisi kwa namna moja au nyingine tunachangia katika uovu. Ukimya wetu katika jambo hili, na mabaya mengine katika jamii zetu, kushindwa kwetu kuheshimu, kushirikiana, mchango wetu katika ukubwa wa familia yenye watoto wengi, sasa hivi tumefungwa na ubinafsi wetu wakujifanya kuwa tumestarabika kwakuwa na mtoto mmoja au wawili basi, kujifungia nakushindwa kuwasaidia wengine, na mambo mengine ambayo yanachangia katika maouvu. Wengine wameogopa kuwa na familia kwa kigezo cha kuogopa kusomesha na badala yake mama anavyoonekana mjamzito hushia kusema ilikuwa haijapangwa nakumtoa mtoto. Tumuombe Mungu atupe neema ya kulinda uhai wa wanadamu mwenzetu tangu alivyo anza kutungwa mimba hadi Mungu atakavyo mchukua mwenyewe.

Tunaomba sikukuu hii-ituletee neema ya kuheshimu aina zote za uhai na neema ya kuhifadhi utu na heshima yakila mmoja wetu..

Sala:Bwana, tusaidie tupende uhai wetu na wa wengine. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni