Alhamisi, Julai 15, 2021
Alhamisi, Julai15, 2021.
Juma la 15 la Mwaka
Kut 3:13-20;
Zab 105:1, 5, 8-9, 24-27;
Mt 11:28-30
MWALIKO KUTOKA KWA YESU
“Kuna kitu zaidi katika maisha” “Bwana lazima atakuwa na mpango na mimi”. Maneno haya tumeyazoea katika maisha yetu, maneno ambayo huonekana mara nyingi kwa wale ambao huonekana kutokuwa na furaha katika maisha. Ni maneno ya wale wanaotafuta maana ya maisha yao.
Mwaliko kutoka kwa Yesu, “njooni kwangu ninyi nyote mnao sumbuka na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha”, ni maneno ambayo tunayasikia daima. Ni maneno ya faraja yenye kutualika tumkaribishe Yesu aangaze maisha yetu ya kila siku, achukue hofu zetu, kuchanganyikiwa kwetu, na yote tuliobeba ambayo yanatuangusha chini. Ni mwaliko wa upendo na huruma na ni mwaliko ambao tunapaswa kuukubali kila siku.
Ni kitu gani kinacho kuelemea? Ni kitu ghani kinacho kufanya uzidiwe na mizigo kiasi ambacho kinakuweka daima katika machungu, kukosa Amani na uwa na hofu nyingi? Je, kuna kitu ambacho unakifikiria sana? Je, kuna kitu ambacho unaona kabisa huwezi hata kukigusa? Chochote kile ambacho kina sumbua moyo wako, Yesu anataka kukinyanyua. Mara nyingi tunabeba mizigo mingi katika maisha ambayo hatutaki kuiachia iondoke. Tunakuwa na hofu ya kumkaribisha Yesu aingie ndani mwetu. Kuja kwa Yesu inamaana kwamba kuwa tayari kuyakabili yote katika hali ya kweli na uawazi na kukabili mizigo yetu mbele ya Yesu. Lakini kitu kikubwa ambacho tunapaswa kufahamu ni kwamba Yesu ni mpole, mwenye huruma, mkarimu katika kusamehe na neema. Yeye anatamani kubeba mizigo yetu juu zaidi hata zaidi ya jinsi tunavyopenda yeye ainyanyue. Yeye anaona ukandamizaji wote na anatamani daima kuuondoa.
Tafakari leo kuhusu huu wito wa Yesu wa upole “Njoo kwangu” bila kuwa na hofu na wasi wasi. Mgeukie yeye na muache yeye aweze kuchambua vitu peke yake. Yeye Anakupenda zaidi ya jinsi unavyo dhani na yeye ataiweka miguu yako katika njia iliyo sawa. Fungua moyo wako kwa Yesu. Tembea katika kiini cha Bwana katika sala na kutana naye katika Ekaristi. Sikiliza wito wake.
Sala:
Bwana, ninakuja kwako na ninaleta kila mzigo wangu kwako. Ninakupa maisha yangu, matumaini yangu, hofu zangu, wakati wangu wote wa sasa na ujao, na hofu zote katika maisha. Yesu ninakupa kila kitu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni